Fusarium mangiferae
Kuvu
Ugonjwa huu unasababishwa na kuvu anayefahamika kitaalamu kama Fusarium mangiferae. Hitilafu za mmea hupatikana zaidi kwenye miche michanga. Miche hutoa vichipukizi vidogo vyenye majani madogo yenye magamba, vikiwa na muonekano ulio mithili ya shada la maua au majani kwenye kilele cha shina. Miche inabaki kuwa iliyodumaa na hatimaye hufa. Utofauti kwenye vitawi vya maua unaweza kuonekana kwenye hitilafu ya maua. Vitawi vya maua vilivyoathirika kwa kiasi kikubwa vinakuwa vimegandana na kusongamaana pamoja kutokana na uwepo wa maua makubwa. Mimea iliyoathirika huanza kuwa na hitilafu zenye msongamano wa vishina na maua. Sehemu zinazokua kama vile majani na machipukizi ya shina huzalisha vishina venye umbo lisilo la kawaida huku vikiwa na vifundo vilivyokaribiana pamoja majani magumu lakini yanayovunjika kirahidi. Majani huwa madogo sana ikilinganishwa na ya mimea yenye afya. Ukuaji wa kawaida na ule wenye hitilafu unaweza kutokea kwa pamoja kwenye mmea.
Tumia mchanganyiko wa majani ya Datura stramonium (Alkaloidi), Calotropis gigantea na mwarobaini (Azadirachtin) ili kupunguza maambukizi. Kuvu anayefahamika kitaalamu kama Trichoderma harzianum pia wana ufanisi katika kudhibiti ukuaji wa vimelea vya ugonjwa. Mimea yenye ugonjwa inapaswa kuteketezwa. Tumia vifaa vya kilimo visivyo na ugonjwa. Vitawishina vya kubebesha kutoka kwa miti iliyoathirika havipaswi kutumika.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na tiba za kibaiolojia, ikiwa zinapatikana. Dawa ya Captan 0.1% husaidia kudhibiti kuenea kwa ugonjwa. Pulizia dawa za kuua wadudu za folidol au metasystox kama hatua ya udhibiti. Pulizia carbendazim 0.1% kwa vipindi vya siku 10, 15, au 30 wakati wa hatua ya kutoka maua. Naphthalene Acetic Acid (NAA) kwa kiwango cha 100 au 200 ppm hupunguza matukio ya ugonjwa katika msimu unaofuata. Kupulizia dawa zenye madini yanayopatikana kwa uchache kwenye tishu hai imethibitika kuwa na uwezo wa kudhibiti au kupunguza tatizo hili.
Ugonjwa huu huenezwa hasa kupitia nyenzo za mimea zilizo ambukizwa. Unyevu wa ziada kwenye udongo, mashambulizi ya utitiri, maambukizi ya kuvu, virusi, madawa ya kuua magugu na kemikali nyingine zenye sumu huchangia katika kuzalisha kuvu. Upungufu wa madini ya chuma, zinki na shaba vilevile unaweza kusababisha hitilafu kwenye mmea. Ugonjwa huenea polepole ndani ya mashamba yaliyoathirika. Joto la nyuzi 10 hadi 15°C husaidia ukuaji wa ugonjwa wakati wa mimea kutoa maua.