Kahawa

Madoa ya Kahawa

Mycosphaerella coffeicola

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa ya kahawia yenye maduara yenye mwanga wa manjano kwenye majani, madogo zaidi kwenye mbegu au matunda.
  • Maambukizi makali husababisha kudondoka mapema kwa majani na kukauka kwa shina.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Kahawa

Kahawa

Dalili

Madoa ya mviringo yenye rangi ya kahawia hafifu/kijivu katikati, yaliyozungukwa na pete pana za kahawia iliyokoza na maduara yenye mwanga wa manjano, yenye ukubwa wa takriban 15 mm huonekana kwenye majani. Madoa mara nyingi huonekana kati ya vijishipa na pia kwenye kingo za majani. Wakati mwingine madoa hukua na kuwa madoa makubwa yasiyo na umbo maalumu, na baka la jani hutokea. Hii mara nyingi hutokea katika maeneo yenye ubaridi na unyevu nyevu na mwinuko wa zaidi ya mita 600 juu ya usawa wa bahari. Madoa kwenye matunda ya kahawa mara nyingi ni madogo, takriban 5 mm kwa upana, lakini wakati mwingine yanaweza kufunika tunda lote. Kwa jumla, hayana umbo maalumu kulinganisha na madoa ya kwenye majani, na hususani kwenye upande ulio wazi kwa jua. Katika hali mbaya ya maambukizi, kudondoka mapema kwa majani na kukauka kwa mashina kunaweza kutokea.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hadi sasa, hakuna suluhisho la udhibiti wa kibaiyolojia linaloonekana kupatikana dhidi ya ugonjwa huu. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua lolote.

Udhibiti wa Kemikali

Wakati wote zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiyolojia ikiwa yanapatikana. Ikiwa inahitajika, tumia bidhaa kama shaba au triazoles. Tumia dawa za kupulizia za shaba kwa miezi mitatu kuanzia wakati wa kutoka maua. Tafadhali kumbuka kwamba dawa za kuua kuvu za shaba zinaweza kuua wadudu wanaokula wadudu waharibifu.

Ni nini kilisababisha?

Madoa haya husababishwa na kuvu Mycosphaerella coffeicola. Kuvu huyu hupendelea vipindi vya unyevu wa juu, mvua nyingi, hali ya joto la juu, na mfadhaiko wa kiangazi (kipindi ambacho mimea huhitaji maji mengi kuliko yanayopatikana), hususani baada ya hatua ya maua.Vimelea huishi kwenye mabaki ya majani. Vijimbegu vya kuvu husambazwa kwa njia ya upepo na matone ya mvua, na kupitia harakati za binadamu kwenye mashamba, hususani wakati mimea ina unyevu na inahitaji maji ili kuota. Miti michanga na isiyo na kivuli ndiyo iliyoko hatarini zaidi.


Hatua za Kuzuia

  • Panga vitalu vya miche kwa nafasi ya kutosha na upitishaji mzuri wa hewa, na kivuli cha takriban 35-65%.
  • Toa virutubisho vya kutosha, hususani nitrojeni na potasiamu.
  • Tengeneza mfumo mzuri wa upitishaji/utoaji maji shambani.
  • Katika mashamba, hakikisha unapunguza mfadhaiko wa mimea (hali ya mmea kukua katika mazingira yasiyo rafiki, k.m, kukosekana kwa maji na virutubisho vya kutosha, na pia uwepo wa maji mengi kupita kiasi shambani) kwa kuongeza virutubisho vilivyopendekezwa na kutengeneza mfumo mzuri wa upitishaji maji.
  • Pogoa mimea ili kuruhusu mtiririko wa hewa kwenye taji.
  • Ondoa mabaki ya miti iliyo pogolewa kutoka shambani ili kuzuia uwezekano wa maambukizi.

Pakua Plantix