Colletotrichum spp.
Kuvu
Aina ya mazao, aina ya mbegu na hali ya kimazingira itaathiri ukali wa dalili. Vidonda vya rangi ya kijivu huonekana kwenye majani, shina, maganda ya mbegu au matunda. Madoa haya yanaweza kuwa na umbo la duara, mviringo au yasiyo na umbo maalumu na yenye kingo za kahawia iliyokolea, nyekundu au zambarau. Ikiwa hali ya hewa ni rafiki, madoa huwa mengi zaidi, huongezeka ukubwa na kuungana, yakigeuka rangi kuwa kahawia iliyokolea au nyeusi wakati wa mchakato. Kitovu(eneo la katikati) chake polepole huwa kijivu na, katika hatua za baadaye za maambukizi, inaweza kuonyeshavimadoa vidogo vyeusi vilivyotawanyika. Kubadilika kwa rangi nyekundu ya mgongo wa majani pia ni kawaida katika baadhi ya mazao. Ugonjwa ukiwa mkali zaidi, majani hunyauka, kukauka na kuanguka, na kusababisha mmea kupukutisha majani mapema. Kwenye mashina, vidonda hurefuka, huchimbika na rangi ya hudhurungi, pia na kingo zenye weusi. Kadri vinavyozidi kuongezeka ukubwa, vidonda vinaweza kuzunguka kitako cha shina, na kusababisha mmea kunyauka na kuanguka. Kufa kwa sehemu ya juu ya shina au matawi pia ni kawaida.
Kuenea kwa ugonjwa kunaweza kuzuiwa kwa kutumbukiza mbegu kwenye maji ya moto kabla ya kupanda (joto na muda hutegemea aina ya zao). Mafuta ya mwarobaini yanaweza kunyunyiziwa. Wakala wa kibaolojia wanaweza pia kusaidia kudhibiti maambukizi. Bidhaa zinazotokana na kuvu Trichoderma harzianum na bakteria Pseudomonas fluorescens, Bacillus subtilis au B. myloliquefaciens pia zinaweza kutumika kama sehemu ya matibabu ya mbegu. Michanganyiko ya shaba iliyoidhinishwa kikaboni inaweza kunyunyiziwa dhidi ya ugonjwa huu katika mazao mbalimbali mara tu dalili zitakapogunduliwa.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Nyunyizia dawa mapema asubuhi, na epuka matumizi ya dawa wakati wa jua kali. Pia, tibu mbegu kabla ya kupanda. Kutibu mbegu kunaweza kutumika kuua kuvu/fangasi kabla ya kupanda. Dawa za kuua kuvu zenye azoxystrobin, boscalid, chlorothalonil, maneb au prothioconazole zinaweza kunyunyiziwa ili kupunguza hatari ya maambukizi (tafadhali zingatia maandalizi na mapendekezo mahususi kwa zao husika). Baadhi ya matukio ya usugu/ukinzani kwa baadhi ya bidhaa hizi yameelezwa. Katika baadhi ya mazao, hakuna matibabu madhubuti yanayopatikana. Hatimaye, matibabu ya baada ya kuvuna pamoja na nta ambayo infaa kwenye vyakula inaweza kutumika ili kupunguza maambukizi kwenye mazao/matunda ambayo yanapaswa kusafirishwa nje ya nchi.
Dalili za ugonjwa huu husababishwa na aina kadhaa za kuvu/fangasi wa jamii ya Colletotrichum spp. Wanaishi kwenye udongo, kwenye mbegu, au kwenye uchafu wa mimea na kwenye aina mbadala ya mimea inayoweza kushambuliwa na kuvu hawa kwa muda wa miaka minne. Kuna njia mbili ambazo maambukizi hupitishwa kwenda kwenye mimea mingine. Maambukizi ya msingi hutokea wakati chavua za kwenye udongo au mbegu zinapoambukiza miche wakati wa kuota na kukua taratibu kwenye tishu za mmea. Katika namna nyingine, chavua hudondoshewa kwenye majani ya chini ya mmea kupitia matone ya mvua na kuanza maambukizi ambayo huenea juu. Maambukizi ya upili huanza wakati chavua zinazozalishwa ndani ya jani au vidonda vya matunda hutawanywa na matone ya mvua, umande, wadudu wanaofyonza au wafanyakazi wa shamba kwenye sehemu za juu za mimea au kwa mimea mingine. Joto la chini au wastani (20 hadi 30 °C), udongo wenye pH ya juu, unyevunyevu wa majani kwa muda mrefu, mvua za mara kwa mara na kivuli kikubwa huvutia ugonjwa huu. Mbolea iliyowekwa kwa uwiano mzuri hufanya mazao kuwa na uwezekeno mdogo sana wa kushambuliwa na Chule.