Nyanya

Kinyaushi cha Miche

Pythium spp.

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Mbegu huoza kwenye udongo.
  • Vidonda vilivyolowana maji vikiwa na rangi ya giza kwenye kitako cha miche.
  • Ukuaji mwepesi ulio mithili ya ukungu hufunika miche.

Inaweza pia kupatikana kwenye

37 Mazao
Shayiri
Maharage
Mung'unye
Kabichi
Zaidi

Nyanya

Dalili

Kinyaushi kinaweza kutokea katika awamu mbili wakati wa ukuaji wa miche, mosi wakati ambao miche haijachomoza au baada ya kuota. Katika awamu ya kabla ya kuota, kuvu hutawala mbegu mara tu baada ya kupanda, na kusababisha kuoza kwa mbegu na kuzuia kuota. Katika awamu ya baada ya kuota, miche hukua katika hali ya udhaifu na kitako cha shina huanza kuoza. Shina huonekana kama laini na lenye utelezi huku kukiwa na vidonda vyenye maji maji, rangi ya kijivu, ya kahawia au nyeusi. Mimea michanga au miti hubadilika rangi na kuanza kunyauka, hatimaye kuanguka chini, huku ukionekana kana kwamba imekatwa kwenye kwenye kitako. Kutokea kwa vitu mithili ya ukungu mweupe au wa kijivu huonekana kwenye mimea iliyokufa au juu ya uso wa udongo. Ikiwa kuna upoteaji au uharibifu mkubwa wa miche, basu upandaji upya unaweza kuhitajika.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Dawa za kibailojia za kuua zinazotokana na kuvu Trichoderma viride, Beauveria bassiana au bakteria Pseudomonas fluorescens na Bacillus subtilis zinaweza kutumika kutibu mbegu au kupakwa kuzunguka eneo la mizizi wakati wa kupanda ili kuzuia au kudhibiti utokeaji mapema wa ugonjwa wa kinyaushi. Katika hali fulani, matibabu ya kuzikinga mbegu kwa kutumia dawa za kuua kuvu za shaba kama vile copper oxychloride au mchanganyiko wa Bordeaux husaidia kupunguza athari na ukali wa ugonjwa huo. Mchanganyiko uliotengenezwa nyumbani unaotokana na dondoo za mimea ya Eupatorium cannabinum huzuia kabisa ukuaji wa Kuvu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi, kwa kutumia hatua zote mbili za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Hatua za kuzuia na mwenendo makini wakati wa shughuli za shamba ni njia bora ya kuepuka ugonjwa huo. Katika mashamba yenye historia ya ugonjwa wa Kinyaushi cha Miche au matatizo ya mfumo wa utoaji maji, basi zingatia kutumia dawa za kuua kuvu kama hatua za kinga. Matibabu ya mbegu kwa kutumia metalaxyl-M yanaweza kutumika kudhibiti utokeaji mapema wa aina kinyaushi cha miche. Kutumia dawa za kupulizia majani zenye captan 31.8% au metalaxyl-M 75% wakati wa hali ya hewa ya mawingu kunaweza pia kusaidia. Udongo au kitako cha mmea vinaweza kuingizwa/kuloweshwa kwa copper oxychlorid au captan kila wiki mbili kuanzia wakati wa kupanda.

Ni nini kilisababisha?

Ugonjwa wa Kinyaushi unaweza kuathiri mazao kadhaa na husababishwa na kuvu jamii ya Pythium, ambao wanaweza kuishi kwa miaka kadhaa katika udongo au mabaki ya mimea. Kuvu hawa hustawi wakati hali ya hewa ni ya joto na mvua, huku udongo ukiwa na unyevu kupita kiasi na mimea ikiwa imepandwa kwa kusongamanisha. Hali zinazoleta athari kwa mimea, kama vile maji kutuama au uwekaji mwingi wa mbolea ya naitrojeni, hudhoofisha mimea na pia huchochea ukuaji wa ugonjwa. Vijimbegu (viiniyoga) vya Kinyaushi cha Miche husambazwa kupitia zana au vifaa vya kilimo vyenye vijidudu vya ugonjwa na tope linalokuwa kwenye nguo au viatu. Ingawaje wanaweza kushambulia mazao wakati wa mzunguko wa maisha yao yote, mbegu zinazoota au miche michanga huwa kwenye hatari zaidi ya thirika zaidi. Ugonjwa si lazima ubebwe kutoka msimu mmoja hadi mwingine mahali pamoja, lakini hutokea zaidi wakati na mahali ambapo kuna hali inayochochea maambukizi.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu kutoka kwenye mimea yenye afya au kutoka kwenye vyanzo vilivyoidhinishwa.
  • Tumia aina ya mbegu zilizo sugu dhidi ya magonjwa ikiwa zinapatikana.
  • Tumia vitalu vilivyoinuliwa kwenye maeneo yanayotuamisha maji au yenye udongo ulio chepechepe.
  • Weka nafasi pana kati ya shimo na shimbo la mbegu au kati ya mche na mche wakati wa kupanda ili kuwezesha ukaukaji wa kanopi.
  • Usipande miche kwa kwenda chini sana wakati wa kupandikiza.
  • Ondoa mimea iliyoambukizwa mara dalili za mwanzo zinapoonekana.
  • Panga utumiaji wa mbolea kwa uwiano ulio sawa na weka mbolea ya naitrojeni kidogo dogo kwa vipindi tofauti badala ya kuweka mbolea nyingi kwa mara moja.
  • Mwagilia mara kwa mara lakini juu juu tu ya udongo.
  • Mwagilia mapema asubuhi ili udongo uwe umeshakauka inapofika jioni.
  • Panga kufanya njia ya umwangiliaji wa pete ili maji yasigusane moja kwa moja na shina.
  • Jihadhari usisafirishe tope bila kukusudia kutoka shamba moja hadi jingine.
  • Takasa (safisha) kabisa zana na vifaa vya kilimo kwa kutumia jiki.
  • Ondoa na haribu mabaki ya mimea baada ya mavuno.
  • Panga mzunguko wa mazao na mimea isiyo na uwezekano wa kushambuliwa.
  • Ikiwezekana, achia wazi udongo wa vitalu ili upigwe na mionzi ya jua kwa kutumia matandazo ya plastiki.

Pakua Plantix