Alternaria solani
Kuvu
Ikiwa mmea una ukungu/bakajani wahi, utaonyesha dalili kwenye majani yake ya awali, shina na viazi. Kutakuwa na madoa ya kijivu au kahawia kwenye majani ambayo huongezeka na kuwa makubwa kama miduara yenye uangavu katikati, ambayo huonekana kama mboni (tabia ya "jicho la fahali/ng`ombe dume"). Madoa pia huzungukwa na upete wa manjano angavu. Ugonjwa unapozidi kuwa mbaya, jani lote linaweza kugeuka njano na kuanguka, na kuacha mmea na majani machache. Wakati majani yanaanguka, viazi chini huweza kuungua na kuwa na rangi kama ya ngozi iliyo ungua na jua. Aina hiyo hiyo ya madoa yenye kitovu angavu pia huonekana kwenye shina na viazi. Viazi vinaweza kuanza kuoza na kujiachia kutoka kwa mmea/shina.
Matumizi ya bidhaa zenye Bacillus subtilis au dawa za ukungu zenye msingi wa shaba zilizosajiliwa kama za kikaboni zinaweza kutibu ugonjwa huu.
Daima ni vizuri kujaribu kuzuia ugonjwa huo na kutumia matibabu ya kibaiolojia ikiwa inawezekana. Kuna dawa nyingi tofauti za ukungu ambazo zinaweza kutumika kudhibiti ukungu/bakajani wahi. Bidhaa hizi zina kemikali kama vile azoxystrobin, pyraclostrobin, difenoconazole, boscalid, chlorothalonil, fenamidone, maneb, mancozeb, trifloxystrobin, na ziram. Ni vizuri kutumia dawa yenye kemikali tofauti katika wakati tofauti . Hakikisha unaweka dawa kwa wakati na kuzingatia hali ya hewa. Hakikisha umeangalia ni muda gani unahitaji kusubiri kabla ya kuvuna viazi/mazao kwa usalama baada ya kutumia dawa hizi
Kuvu/fangasi aina ya Alternaria solani husababisha dalili za ugonjwa huu. Wanaweza kuishi kwenye udongo, kwenye uchafu wa mimea iliyoambukizwa au kwenye mimea mingine wakati wa baridi. Unaweza pia kupata mimea iliyoambukizwa kwa kununua mbegu ambayo tayari ina vimelea. Majani ya chini mara nyingi huambukizwa wakati yanapogusa udongo wenye vimelea. Kuvu hawa hukua vizuri zaidi kunapokuwa na joto (24-29°C) na unyevunyevu mwingi (90%). Kipindi kirefu cha hali ya hewa ya mvua au hali ya hewa ya unyevu na ukame inaweza kusaidia kuvu kutoa mbegu/chavua, ambazo zinaweza kuenezwa na upepo, mvua, au umwagiliaji wa juu. Kwa zao la viazi, viazi vya kijani vina uwezekano mkubwa wa kuambukizwa na kuvu. Ugonjwa huo mara nyingi huonekana baada ya mvua kubwa na huharibu hasa katika maeneo ya tropiki na ya joto.