Phyllachora maydis
Kuvu
Dalili za awali zina sifa ya kuwa madoa madogo, yaliyoinuka yakiwa na rangi ya manjano-kahawia yenye weusi katikati kwenye pande zote za jani. Madoa haya yanaweza kuzungukwa na vidonda vya mviringo, vya rangi ya kahawia vilivyo na kingo za giza, vinavyojulikana kama "jicho la samaki." Madoa ya mviringo, umbo la yai wakati mwingine yakiwa na umbo pembe au yasiyo ya umbo maalumu yanaweza kuungana na kuunda mistari yenye urefu wa hadi milimita 10. Jani zima linaweza kufunikwa na madoa, na sehemu ya jani inayozunguka madoa haya hukauka. Dalili hutokea kwanza kwenye majani ya chini, kisha kuenea hadi kwenye majani ya juu. Kama mashambulizi ni makubwa, madoa haya pia yanaweza kuonekana kwenye kifuko cha majani. Majani yanaweza kufa kabisa baada ya siku 21 hadi 30, jambo linaloweza kusababisha kupungua kwa ubora wa mazao kwenye soko.
Hakuna suluhisho la udhibiti wa kibaolojia linaloonekana kupatikana dhidi ya ugonjwa huu. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua lolote.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye kutumia hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaolojia ikiwa yanapatikana. Hadi leo, hakuna tiba ya kemikali inayojulikana kwa ugonjwa huu. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua tiba yoyote.
Dalili husababishwa na mwingiliano wa aina tatu za kuvu ambao wanafahamika kitaalamu kama: Phyllachora maydis, Monographella maydis, na hyperparasite Coniothyrium phyllachorae. Siku mbili au tatu baada ya maambukizi na P. maydi , vidonda huvamiwa na M. maydis. Kuvu hawa wanaweza kuishi kwenye mabaki ya mimea kwa miezi 3 au zaidi. Vijimbegu vya kuvu vinaenezwa na upepo na mvua. Halijoto ya ubaridi a 16-20°C na unyevunyevu anga wa juu huchochea mlipuko wa ugonjwa. Kwa hivyo, mashamba yaliyo karibu na kingo za mito yapo hatarini kushambuliwa na ugonjwa huu.