Mahindi

Ubwiri Vinyoya wa Mahindi

Peronosclerospora sorghi

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Kutokea kwa mistari ya manjano kwenye majani.
  • Muonekano wa kudumaa na mithili ya kichaka.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mahindi

Dalili

Utokeaji wa ukuaji wa vinyoya vyeupe kwenye sehemu ya juu na ya chini ya majani. Ufupi wa pingili kati ya kifundo na kifundo kwenye shina husababisha mimea iwe na mwonekano wa kudumaa na mithili ya vichaka. Ukuaji wa vinyoya pia hutokea kwenye bract (jani lililobadilishwa) ya maua ya kijani ya kiume yasiyofunguliwa kwenye ua la kiume. Majani madogo hadi makubwa yanaonekana kwenye sehemu ya kiume ya ua.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Panda mbegu zinazostahimili magonjwa na mbegu chotara.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye kutumia hatua za kinga na matibabu ya kibaolojia yanayopatikana. Tibu mbegu kwa kutumia dawa za kuua kuvu zinazofyonzwa na mmea zenye viambato hai kama metalaxyl na mancozeb.

Ni nini kilisababisha?

Madhara husababishwa na kuvu, ambae hukua kama vinyoya vyeupe kwenye pande zote mbili za majani. Chanzo kikuu cha maambukizi ni kupitia viinimbegu vilivyozalishwa kutokana na urutubishaji wa vijiyai (ova) vya kuvu kwenye udongo na kutokana na kuvu bwete/tuli weupe walio mithili ya mtandao wa mizizi (yaani, mycelium) iliyopo kwenye mbegu za mahindi zilizoathirika. Mara baada ya kuvu kuingia kwenye tishu ya mmea unaohifadhi vimelea, sporangiophores huibuka kutoka kwenye stomata na kuzalisha vijimbegu vya kuvu visivyojongea ambavyo huenezwa na mvua na upepo, na kusababisha maambukizi ya upili.


Hatua za Kuzuia

  • Fanya kilimo safi.
  • Lima kwa kuchimbua udongo.
  • Tumia kilimo cha mzunguko wa mazao na mimea ya jamii ya mikunde.
  • Ondoa mimea iliyoathirika.

Pakua Plantix