Choanephora cucurbitarum
Kuvu
Dalili za awali zinajulikana kwa weusi na kunyauka kwa maua, vitumba vya maua au sehemu zinazokua (mabaka ya maua). Ugonjwa huu kisha huenea kuelekea chini, na kusababisha vidonda vyenye unyevu/majimaji kwenye majani, na kuyapa rangi mithili ya fedha. Vidonda vya zamani hubadilika na kuonekana vimekauka kutokana na kufa kwa tishu (nekrotiki), na kusababisha mabaka kwenye ncha na kingo za majani. Kwenye mashina, ishara za kuoza zinaonekana kwa namna ya madoa ya kahawia hadi meusi na kunyauka. Hatimaye, mmea mzima unaweza kunyauka. Uozo laini mweusi unaweza pia kutokea kwenye matunda machanga, kwa kawaida kwenye ncha ya maua. Uchunguzi wa karibu utaonyesha ukuaji wa vitu vya rangi mithili ya rangi ya fedha, unaofanana na nywele kwenye tishu zote zilizoathiriwa. Kwenye miche, dalili zinaweza kuchanganywa na mabaka ya Phytophthora.
Hakuna matibabu ya kibaiolojia yanayopatikana kwa ugonjwa huu. Huko Benin, bakteria Bacillus subtilis wamejaribiwa kwa mafanikio kwa baadhi ya mazao kwa athari yake dhidi ya Choanephora cucurbitarum. Hata hivyo, hakuna jaribio lolote lililofanywa kwenye pilipili.
Wakati wote zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiyolojia, ikiwa yanapatikana. Kuzuia ni muhimu kwani hakuna dawa za kuua kuvu zilizothibitishwa kwa ajili ugonjwa huu. Udhibiti kwa kutumia dawa za kuua kuvu kunaweza kusaidia kupunguza maendeleo ya dalili lakini mara nyingi ni vigumu kwa sababu mimea inaendelea kuchanua maua na hivyo kuwa hatarini kuathirika na vimelea vya magonjwa.
Dalili hizi husababishwa na Choanephora cucurbitarum, kuvu anayeshambulia zaidi tishu ambazo zimeharibiwa na wadudu au kwa njia za mitambo wakati wa kazi ya shambani. Kwa ujumla, vijimbegu vyake husambazwa kwa njia ya upepo, maji yanayoruka, na kupitia nguo wakati unagusana na zana pamoja na vifaa vya kilimo. Milipuko ya ugonjwa huu kwa kawaida hutokea wakati wa vipindi virefu vya mvua, unyevunyevu wa juu na joto la juu. Si ajabu kwamba inasababisha uharibifu mkubwa kwa pilipili na bamia zinazolimwa wakati wa msimu wa mvua katika maeneo ya kitropiki. Mazao ambayo hayajaendana vizuri na hali hizi yatakuwa hatarini zaidi kuathirika. Ili kutofautisha na mabaka ya Phytophthora, chunguza tishu kuona uwepo wa nywele za kijivu (hasa asubuhi).