Pilipili Hoho & Pilipili

Ubwiri Unga wa Pilipili

Leveillula taurica

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Poda/unga, madoa meupe kwenye sehemu ya chini ya majani na madoa ya njano upande wa juu.
  • Dutu ya unga unga kwenye majani inayoweza kufutika.
  • Sehemu zilizoambukizwa husinyaa, majani huanguka.
  • Mmea unaweza kufa.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Pilipili Hoho & Pilipili

Dalili

Leveillula huathiri zaidi majani wakati mabua na matunda huambukizwa mara kwa mara. Dalili za mwanzo ni unga, madoa meupe kwenye sehemu ya chini ya majani na madoa ya njano yenye ukubwa tofauti upande wa juu. Baadaye, madoa meupe, ya unga yanaweza pia kutokea upande wa juu. Ugonjwa unapoendelea, sehemu zilizoambukizwa husinyaa, majani huanguka na mimea inaweza kufa.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Kwa bustani, miyeyuko ya maji na maziwa inaonekana kufanya kazi kama dawa ya asili ya kuua kuvu. Weka mchanganyiko huo kwenye majani kila siku ya pili. Aina za ubwiri unga hutofautiana kulingana na mazao, na mchanganyiko huo hauwezi kuwa na ufanisi kwa kila aina. Ikiwa hakuna mabadiko ya wazi, jaribu vitunguu swaumu au kimimika cha bikarboneti ya sodiamu(soda ya kuoka). Tiba za kibayolojia za kibiashara zinapatikana pia.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Kwa sababu idadi kubwa ya mazao huathiriwa na ubwiri unga, ni vigumu kupendekeza matibabu maalum ya kemikali. Dawa za kuua kuvu zenye salfa yenye unyevunyevu, triflumizole, myclobutanil, zinaonekana kudhibiti ukuaji wa fangasi katika baadhi ya mazao.

Ni nini kilisababisha?

Vijidudu vya kuvu husali msimu mzima ndani ya machipukizi ya majani na uchafu mwingine wa mimea. Upepo, maji na wadudu husambaza vijimbegu/chavua kwenye mimea iliyo karibu. Ingawa ni Kuvu, ubwiri unga unaweza kukua kwa kawaida katika hali kavu. Hustahimili joto kati ya 10-12 ° C, lakini hali bora hupatikana kwa 30 ° C. Tofauti na ubwiri vinyoya/sufi, kiasi kidogo cha mvua na umande wa asubuhi wa kawaida huharakisha kuenea kwa ubwiri unga.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina sugu au zinazostahimili.
  • Panda mimea kwa nafasi ya kutosha ili kuruhusu uingizaji hewa mzuri.
  • Ondoa majani yaliyoambukizwa wakati madoa ya kwanza yanapo onekana.
  • Usiguse mimea yenye afya baada ya kugusa mimea iliyoambukizwa.
  • Safu nene ya matandazo inaweza kuzuia kuenea kwa vijimbegu kutoka kwenye udongo hadi kwenye majani.
  • Katika visa flani, mzunguko wa mazao husaidia.
  • Weka mbolea yenye uwiano mzuri wa virutubisho.
  • Epuka mabadiliko makubwa ya joto.
  • Lima kwa kufunika au ondoa mabaki ya mimea baada ya kuvuna.

Pakua Plantix