Peronospora manshurica
Kuvu
Dalili za awali za Ubwiri nyoya wa Soya hutokea kwenye mimea michanga lakini ugonjwa hauonekani shambani hadi kipindi cha mwishoni cha kuchipua kwa mmea au kwenye hatua za awali za uzazi(kuweka maua). Mwanzoni, madoa madogo, yasiyo na mpangilio, yenye rangi ya njano hafifu huonekana kwenye nyuso za juu za jani. Baadaye, huwa na rangi ya kijivu-kahawia na ukingo wa manjano. Kwenye upande wa chini wa majani, madoa yana mwonekano wa kijivu ulio fifia kutokana na kuwepo kwa vimelea. Dalili mara nyingi hutokea kwa viwango vya chini kwenye sehemu yote ya majani. Wakati maganda ya mbegu yameambukizwa, wingi wa kuvu unaofanana na ukungu huonekana ndani ya maganda. Mbegu iliyoambukizwa ina mwonekano wa rangi nyeupe ya kufifia na imezungukwa na kuvu kwa sehemu au yote kabisa. Ukubwa wa vidonda na umbile hutegemea umri wa jani. Vidonda vya zamani vinaweza kugeuka rangi ya kijivu hadi kahawia iliyokolea na kingo za njano au kijani. Majani yaliyoathirika sana hubadilika kutoka manjano hadi hudhurungi na kudondoka kabla ya wakati.
Mpaka sasa, hatufahamu mbinu yoyote ya udhibiti wa kibayolojia inayopatikana dhidi ya vimelea hivi. Ikiwa unajua njia yoyote iliyofanikiwa ya kupunguza matukio au uzito wa dalili za ugonjwa huu, tafadhali wasiliana nasi.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia, endapo yanapatikana. Weka dawa za kuua kuvu kama vile metalaxyl, oxadixyl pamoja na mancozeb, maneb au zineb kwa matibabu ya mbegu.
Ubwiri nyoya wa Soya husababishwa na viumbe vinavyofanana na fangasi viitwavyo Peronospora manshurica. Huishi shambani msimu mzima wa majira ya baridi kama vijidudu vyenye kuta nene kwenye mabaki ya majani na mara chache kwenye mbegu. Ugonjwa huu mara nyingi hutokea baada ya maua kuanza kutoka. Majani machanga huathirika zaidi na majani yaliyoambukizwa mara nyingi huonekana katika sehemu ya juu ya mimea. Vidonda kwenye mimea mikubwa ya soya vinaweza kuongezeka kwa idadi na kupungua kwa ukubwa kwenye majani yaliyo komaa/kuzeeka. Ugonjwa huu hupendelea joto la wastani (20-22 ° C) na unyevu wa juu. Ubwiri nyoya wa Soya hukaa shambani kama vijimbegu/chavua zenye kuta nene (oospores) kwenye mabaki ya majani na kwenye mbegu. Maendeleo ya ugonjwa hutegemea zaidi hali ya hewa. Unyevu unapopungua, vimelea vya ugonjwa huugua na kuzuia kuenea kwa ugonjwa msimu/siku zijazo. Kwenye uwepo wa unyevu mwingi na mvua za mfululizo, Ubwiri nyoya huendelea kukua.