Pleospora allii
Kuvu
Dalili za awali ni pamoja na madoa madogo, yaliyotota maji, meupe hadi manjano hafifu kwenye majani. Kwa kawaida, vidonda hivi hupatikana kwa idadi kubwa zaidi upande wa majani yanayotazama kwenye uelekeo wa upepo. Baada ya muda, vidonda hivi vidogo hukua sambamba na bapa ya jani na kuungana na kuwa madoa ya hudhurungi yaliyozama, yenye umbo la mviringo au marefu, yenye rangi ya hudhurungi. Kanda zenye kitovu cha pamoja zinaweza pia kutokea katikati ya madoa hayo. Katika hatua za juu, maeneo makubwa yenye seli/tishu zilizokufa huundwa, ambayo yanaweza kulifunga jani au shada la mbegu, na kusababisha baka kubwa kwenye tishu.
Vimiminika vya mwarobaini(Neem) na mchawasha (jimsonweed) vinaweza kutumika kwa udhibiti wa kibayolojia wa ugonjwa wa bakajani Stemphylium la Vitunguu kwa ufanisi unaokaribia ule wa viua kuvu vya kiwandani. Chini ya hali ya kwenye kitalu nyumba, matumizi ya kinga au tiba ya bidhaa zenye Trichoderma harzianum na Stachybotrys chartarum husababisha kupungua kwa matukio na ukali wa ugonjwa (karibu 70% katika visa vyote viwili).
Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kuzuia na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Kimiminika chenye viambato hai vya azoxystrobin + difenoconazole, boscalid + pyraclostrobin, chlorothalonil, iprodione, mancozeb na prochloraz ni bora sana katika kupunguza ukuaji wa S. vesicarium. Matibabu yanapaswa kufanyika wakati hali ya hewa siyo rafiki kwa kuvu (hali ya hewa tulivu na kavu). Kwa ujumla, ufanisi wa dawa za kuua kuvu huimarishwa endapo utabadilisha dawa/bidhaa.
Ugonjwa wa bakajani Stemphylium husababishwa na kuvu wa Pleospora allii, ambao zamani walijulikana kama Stemphylium vesicarium, na hivyo kupata jina la ugonjwa huo. Wanaishi kwenye mabaki ya mimea iliyoambukizwa na huanza tena ukuaji wakati wa hali nzuri ya hewa katika majira kuchipua. Kisha hutoa vijimbegu ambavyo huenea kwa upepo hadi mimea iliyo karibu. Kwa kawaida huvamia tishu za kitunguu zilizokufa na zinazokufa, kama vile ncha za majani, vidonda vilivyosababishwa na magonjwa ya awali, au tishu zilizojeruhiwa (na wadudu au mvua ya mawe). Muda mrefu wa hali ya joto na mvua huchochea maendeleo ya ugonjwa. Majani yenye afya pia yanaweza kushambuliwa ikiwa hali ya hewa ni ya joto (18 - 25 °C) na uso wa jani ukiwa na unyevu kwa zaidi ya masaa 24. Maambukizi kawaida hubakia tu kwenye majani na hayaathiri kitunguu chenyewe. Majani makongwe yanahusika zaidi kuliko machanga.