Diaporthe vexans
Kuvu
Dalili huonekana kwenye majani, shina, na matunda, na huonekana zaidi kwenye matunda. Madoa madogo ya rangi ya kijivu hadi kahawia, yakiwa machache katikati huonekana kwenye majani na hatimae yanaweza kuwa mengi na kufunika maeneo makubwa ya jani. Majani yaliyoambukizwa sana hugeuka kuwa ya manjano na baadaye kunyauka, yakiwa na tishu zenye nyufa na kuchanika (baka jani). Mashina yanaweza kutengeneza kikwachu (kidonda) cha kahawia hadi rangi ya giza, huku kikiwa na nyufa na kuzama. Katika msingi/kitako cha mmea, kikwachu hiki kinaweza kuzunguka shina na kuzuia usafirishaji wa maji na virutubisho, hatimaye kuua mmea. Vidonda vya kahawia, laini, na vilivyozama huonekana kwenye matunda. Kadri vidonda hivi vinavyoongezeka ukubwa, mara nyingi huungana, na kufunika sehemu kubwa ya uso wa tunda na kutengeneza pete zenye vidoa vidogo vya buluu kwenye kingo zake. Hatimaye, matunda huoza. Vidoa vidogo vyeusi pia huonekana kwenye vidonda vya zamani kwenye majani na mashina. Ikiwa hali inakuwa kavu, matunda yaliyoambukizwa hunyauka, kukauka, na kufia kwenye mmea.
Matibabu kwa kutumia dawa za kuua kuvu za asili yanaweza kuwa na manufaa katika kupunguza uwepo na ukali wa ugonjwa. Dawa zinazotokana na mchanganyiko wa shaba (k.m. mchanganyiko wa Bordeaux) zinaweza kutumiwa kama dawa ya kupulizia majani. Mchanganyiko wa mwarobaini ni suluhisho salama na rafiki kwa mazingira ambalo limekuwa likitumika katika usimamizi wa ugonjwa. Matibabu ya mbegu kwa maji ya moto pia yanaweza kuzingatiwa (56 °C kwa dakika 15).
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Ikiwa ugonjwa unagundulika shambani na faida za kiuchumi zinakidhi, basi inapendekezwa kutibu mimea kwa dawa za kuua kuvu. Dawa maarufu zaidi za kuua kuvu zinazotumiwa kwa kupulizia majani ni azoxystrobin, boscalid, captan, chlorothalonil, copper oxychloride, dithiocarbamates, maneb, mancozeb, thiophanate-methyl, tolclofos-methyl, na pyraclostrobin. Dawa za kuua kuvu zinakuwa na ufanisi zaidi wakati zinapounganishwa na njia za asili za kudhibiti kuvu. Matibabu ya mbegu yanaweza pia kutumika, kwa mfano kwa thiophenate methyl (0.2%).
Dalili zinasababishwa na kuvu aina ya Phomopsis vexans, kimelea kinachoonekana kushambulia zaidi bilinganya (ingawa kumekuwa na ripoti za maambukizi kwenye nyanya na pilipili). Kuvu huyu huishi kwenye mabaki ya mazao na vijimbegu (viioniyoga) vyake husambazwa kwa njia ya upepo na mvua hadi kwenye mimea yenye afya. Pia inadhaniwa kuwa hubebwa ndani na juu ya mbegu. Hii inamaanisha kwamba kupata mbegu zilizothibitishwa na miche yenye afya kuwa ni njia muhimu katika kupambana na ugonjwa huu. Inaweza kuchukua saa 6 - 12 kupenya kwenye tishu za majani, na hali ya joto na unyevu kiasi inahitajika kwa ajili ya maambukizi na maendeleo ya ugonjwa (27-35° C). Maendeleo ya vidonda vya matunda yana uwezekano mkubwa wa kutokea katika 30°C na unyevu wa asilimia 50 katika vyumba vya uhifadhi.