Penicillium spp.
Kuvu
Dalili za awali ni pamoja nakutokea kwa sehemu laini iliyotota/lowana maji kwenye ganda. Baada ya siku chache, doa la kuvu/ukungu mweupe, la mviringo na lililo juu kwenye ganda hukua kwenye kidonda cha awali, mara nyingi likiwa na kipenyo cha sentimita kadhaa. Baada ya muda, ukungu huenea juu juu kwenye ngozi na katikati ya sehemu kongwe hugeuka rangi na kuwa ya kibuluu au kijani. Tishu zilizo karibu zinakuwa laini na zilizotota maji au zinakaliwa na ukanda mpana wa kuvu mweupe anayefahamika kama mycelium, yaani kuvu mithili ya mizizi. Tunda linaharibika haraka na kuporomoka, au katika unyevu mdogo hunywea na kuwa kama mfu.
Udhibiti wa kibaiyolojia wa kuvu unaweza kufanikiwa kwa kutumia michanganyiko inayotokana na aina ya Pseudomonas syringae ESC-10. Dondoo kutoka kwenye mmea wa Ageratum conzyoides pia ina ufanisi dhidi ya ukungu. Mafuta muhimu kutoka kwenye mimea ya Thymus capitatus na mafuta ya mwarobaini yana athari sawa. Saponin ya chai inachukuliwa kuwa mchanganyiko salama na pia imekuwa ikitumika kudhibiti kuoza kwa matunda ya jamii ya machungwa baada ya mavuno.
Daima zingatia mbinu jumuishi zikiwa na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiyolojia ikiwa yanapatikana. Kuosha matunda yaliyovunwa kwa joto la 40-50°C kwa kutumia sabuni au mchanganyiko wa alkali dhaifu, kwa kawaida zikijumuisha baadhi ya dawa za kuua kuvu/ukungu, hupunguza kuoza kwa matunda. Dawa za kuua kuvu zinazopendekezwa ni imazalil, thiabendazole, na biphenyl.
Aina mbili za kuvu/ukungu kutoka jenasi Penicillium husababisha uharibifu wa kuoza kwa matunda ya jamii ya machungwa. P. italicum na P. digitatum hukua kwenye ngozi ya tunda kama ukungu wa buluu na ukungu wa kijani mtawalia. Kwa kawaida vidonda vya P. italicum huenea polepole zaidi kuliko vile vinavyosababishwa na P. digitatum. Ukuaji wake pia hujulikana kwa mkanda wa kuvu mycelium (kuvu mithili ya mizizi ) mchanga mweupe anaezunguka vidonda vilivyo sababishwa na P. italicum katikati. Kuvu hawa ni watumia fursa ya uwepo wa majeraha kwenye uso wa tunda ili kuanzisha mzunguko wao wa maisha. Vijinbegu (Spores) vya kuvu/ukungu huota kwa kuachiliwa maji na virutubisho kutoka kwenye eneo la jeraha. Katika joto muafaka la 24 °C, maambukizi hutokea ndani ya saa 48 na dalili za awali huonekana ndani ya siku 3. Uambukizaji unaweza kutokea kwa njia ya kimekanika au uenezwaji wa vijimbegu vya kuvu kwa njia ya maji au hewa. Vijimbegu hivi mara nyingi hukaa kwenye udongo lakini pia vinaweza kupatikana kwenye hewa ya maeneo ya kuhifadhi yaliyochafuliwa.