Pseudoperonospora cubensis
Kuvu
Licha ya tofauti ndogo kati ya zao moja na lingine, ugonjwa wa Ubwiri Unyoya kwenye mimea jamii ya maboga (maboga, matikiti, matango, n.k) kwa ujumla hutambulika kutokana na kutokea kwa madoa ya manjano, yenye umbo la pembe kwenye upande wa juu wa majani ambayo hayaongezeki kuvuka mishipa mikubwa ya jani. Ubadilikaji huu wa rangi kati ya mishipa, taratibu hutengeneza muundo au nakshi ya mozaiki yenye rangi ya manjano hadi kahawia ambayo haipaswi kufananishwa na maambukizi ya virusi. Kwenye upande wa chini wa jani, vidonda vyenye unyevunyevu vinavyotokea chini ya madoa haya huanza kupata mwonekano wa rangi ya kijivu iliyofifia, laini mithili ya manyoya wakati wa hali ya baridi na unyevunyevu wa muda mrefu. Kadri kuvu (ukungu) unavyonyonya virutubisho kutoka kwenye mmea, inaweza kusababisha udumavu au kufa kwa vishina vidogo, maua, au matunda, na kupelekea ukuaji duni na mavuno hafifu. Tofauti na ukungu aina ya ubwiri unga, ukungu wa ubwiri unyoya hufunika tu upande wa chini wa majani na ukuaji wake huzuiliwa na mishipa mikubwa ya jani. Zaidi ya hayo, hauwezi kuondolewa kwa urahisi.
Matibabu ya kibaiolojia kibiashara kwa ajili ya kupambana na ubwiri unyoya zinapatikana. Katika hali ya maambukizi madogo, mara nyingi ni bora kutofanya chochote na kusubiri hadi hali ya hewa iboreke. Katika mazingira fulani fulani, dawa za kuzia kuvu za kikaboni kabla ya maambukizi zinaweza kusaidia kuzuia maambukizi ya mimea, na dawa hizi ni pamoja na zile zinazotokana na shaba, kama vile mchanganyiko wa Bordeaux.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua kuvu zenye uwezo wa kukinga zinaweza kusaidia kuzuia maambukizi ya mimea, lakini ni lazima zipuliziwe vizuri upande wa chini wa majani. Michanganyiko ya dawa zenye mancozeb, chlorothalonil au misombo inayotokana na shaba inaweza kutumika. Dawa za kuua kuvu zinazotumika baada ya maambukizi ni lazima zitumike mara tu dalili za kwanza zinapogunduliwa. Dawa maarufu za kuua kuvu baada ya maambukizi ni pamoja na mefenoxam, strobilurins, fluopicolide, famoxadone+cymoxanil, cyazofamid, na zoxamide. Usugu kwa baadhi ya dawa hizi umeonekana.
Dalili Ubwiri Unyoya husababishwa na kuvu kutoka kwenye kundi la ukungu wa maji, ambao kitaalamu unafahamika kama Pseudoperonospora cubensis. Hawa ni vijidudu ambao ni lazima wapate mimea wanayoweza kuinyonya ndipo waweze kukamilisha mzunguko wao wa maisha. Ni vijidudu hatari zaidi katika maeneo yenye vivuli na hali ya hewa yenye ubaridi, majimaji, na unyevu (umande mzito, ukungu, usimbishaji) na joto la takriban nyuzi 15-23°C. Kuvu huishi msimu wote wa majira ya baridi kwenye mabaki ya mimea iliyoathirika au kwenye machipukizi au kwenye mimea mbadala (mazao na magugu) ambayo vimelea vya kuvu vinaweza kuishi. Upepo, mkondo wa hewa, na matone ya mvua husambaza vijimbegu (viiniyoga) vya ubwiri unyoya kwenye tishu za mimea yenye afya wakati hali ni nzuri. Mara vinapodondokea kwenye mimea ambayo vinaweza kuishi, vijimbegu hivi huota na kuzalisha maumbile yanayoingia kwenye tishu za mimea kupitia matundu ya asili yaliyo upande wa chini wa majani. Hapo huanza kuenea, na hatimaye huzidi ukuaji wa tishu za ndani na kutengeneza mipako ya ukungu inayoonekana nje. Hapo vijimbegu huzalishwa, ambavyo vitasambaza ugonjwa hata na zaidi.