Alternaria alternata
Kuvu
Dalili kwa ujumla huonekana wakati wa kiangazi na hudhihirishwa na kuwepo kwa madoa yenye pembe au mviringo yenye kipenyo cha milimita 3 hadi 7 kwenye vipande vya majani. Katika hali zingine kali au katika aina zinazoweza kuathiriwa kirahisi, madoa huwa na kipenyo cha hadi 3 cm. Vidonda vyeusi pia huwepo kwenye vikonyo na mishipa mikuu ya ubapa wa majani. Uvamizi mkali unaweza kusababisha majani kunyauka na kuanguka. Kwenye matunda machanga, madoa madogo ya kahawia au meusi yanaonekana. Kwenye matunda yaliyokomaa, madoa ni makubwa zaidi (kipenyo cha mm 1 hadi 5) na yamezungukwa na mduara angavu mwekundu. Ukungu huanza kukua kwenye matunda, na kusababisha kuoza kwake. Katika hali mbaya, hii hupunguza sana ubora wa bidhaa.
Nyunyiza mchanganyiko wa Bordeaux kwenye miti na vipandikizi baada ya kupogoa sehemu zilizoathirika. Vinginevyo, tumia mchanganyiko wa vitunguu saumu au mimea ya mkia wa farasi kwenye majani na matunda. Unaweza kutumia suluhisho la Bacillus subtilis, ambae ni mwindaji wa kuvu.
Daima zingatia usimamizi jumuishi wa wadudu na hatua za kuzuia na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu dhidi ya ugonjwa huu yanapaswa kuanza katika majira ya joto mapema, kabla ya kukomaa kwa matunda. Bidhaa zenye viambato hai vya thiophanate-methyl, maneb, shaba hufanya kazi vizuri. Angalau matibabu mara mbili yanahitajika ili kupunguza maambukizi. Ufanisi wa matibabu hutegemea muda wa matumizi, marekebisho ya umri wa mti, na matumizi ya kipimo kilichopendekezwa.
Dalili husababishwa na kundi la fangasi watatu wa jenasi za Alternaria, miongoni mwa wengine Alternaria alternata. Wanajificha kwenye udongo au kwenye uchafu wa mimea. Wakati hali ni nzuri, hutoa vijimbegu ambavyo husafirishwa na upepo, mvua hadi kwenye miti inayoshambuliwa. Joto la juu linalohusishwa na unyevu wa juu, ikiwa ni pamoja na kutokeai kwa umande, vipindi vya mvua na jua, na upungufu wa virutubisho ni sababu kuu za maendeleo ya ugonjwa kwenye pistachio/mfistiki. Dalili zinaweza kuchanganywa na zile za baka la suke na chipukizi linalosababishwa na Botryosphaeria dothidea. Ili kuwatofautisha, sugua majani yaliyoathiriwa wakati hali ya unyevu inapotawala: ikiwa itafanya vidole kuwa nyeusi, basi huo ni ugonjwa wa baka chelewa unaosababishwa na Alternaria alternata.