Pseudocercospora pistacina
Kuvu
Ugonjwa huu husababisha madoa yenye tishu zilizo kufa ya mviringo hadi yasiyo na umbo la kawaida, rangi ya kahawia hadi kahawia nyeusi, pande zote mbili za majani. Kwenye majani, madoa haya yanaweza kuwa mengi sana na kufikia kipenyo cha 1 hadi 2 mm. Baada ya muda, ubapa wa jani polepole hubadilika kuwa kijani hafifu na baadaye kuwa kahawia, kuanzia pembezoni na kuenea kuelekea katikati. Mashambulizi makubwa yanaweza kusababisha majani kunyauka na kuanguka mapema. Madoa madogo sana yanaweza pia kuundwa kwenye matunda. Milipuko mikali ya ugonjwa huu inaweza kusababisha upukutishaji wa majani mapema na kudhoofisha afya ya miti. Kuanza kwa mashambulizi kwa ujumla huanza mwezi wa nne baada ya viini vinavyopatikana kwenye takataka za majani ya mwaka uliopita kuhamia kwenye mmea.
Katika dalili za awali, nyunyiza bidhaa za shaba au salfa. Matumizi lazima yafanyike baada ya matunda kufikia takriban 1 cm kwa ukubwa ili kuepuka uharibifu wa sumu kwenye matunda machanga sana.
Daima zingatia usimamizi jumuishi wa wadudu na hatua za kuzuia na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Kutokana na kuonekana kwa madoa ya kwanza, nyunyiza mara 2 au 3 bidhaa zilizo na kiambata hai cha thiophanate-methyl. Matibabu na viua kuvu vyenye zineb, mancozeb, chlorothalonil au viua kuvu vya shaba pia yanafaa, lakini lazima yatumiwe baada ya matunda kufikia ukubwa wa 1 cm ili kuepuka uharibifu wa sumu kuvu kwenye matunda machanga sana. Badilisha viambato hai tofauti ili kuzuia ukuaji wa ukinzani/usugu. Matibabu ya kuzuia baada kuchipua pia yanafaa ili kuzuia kuonekana kwa ugonjwa huu.
Dalili husababishwa na fangasi kadhaa wa jenasi ya Mycosphaerella, katika eneo la Mediterania hasa M. pistacina. Huishi kwenye majani yaliyoanguka kwenye takataka za udongo zilizoambukizwa wakati yakiwa kwenye mti katika misimu iliyopita. Uchafuzi wa awali ni kupitia viini ya kuvu kutoka kwenye majani haya. Matone ya mvua husaidia katika kusambaza vijimbegu. Maambukizi ya upili husababishwa na aina nyingine za vijimbegu ambavyo pia huenezwa na mvua au maji ya kunyunyiza, hadi mwishoni mwa msimu. Joto la juu kati ya 20 na 24 ° C, hali ya hewa yenye unyevunyevu na ukungu ni hali nzuri kwa maendeleo na kuzaliana kwa vimelea.