Phyllosticta maculata
Kuvu
Dalili ya tabia kuu ni madoa yenye rangi ya kahawia iliyokolea hadi meusi yenye ukubwa tofauti kwenye majani na matunda. Uso wa jani na maganda ya matunda huonekana kama msasa. Madoa madogo yana kipenyo cha chini ya 1mm. Madoa haya yanaweza kukusanyika katika mistari na kuonekana kama michirizi inayopita kwa mshazari kukatiza jani, au kutoka katika vena kuu (mshipa wa katikati) hadi kwenye ukingo wa jani, mara nyingi kwenye vijishipa jani. Madoa makubwa yana kipenyo cha hadi 4mm na yanaweza pia kuonekana kama michirizi. Wakati mwingine katikati ya madoa haya makubwa kunakuwa na rangi hafifu. Madoa yanaweza pia kutokea kwenye vikonyo, vena kuu za majani, majani ya mpito na bracts(jani lililobadilishwa na kuwa mithili ya sepali). Matunda pia yanaweza kuathiriwa na mabaka kunako mapema kiasi cha wiki 2-4 baada ya mkungu kuibuka. Doa moja moja hutokea kwanza kama vijidoa vidogo vya rangi ya kahawia yenye wekundu vilivyozungukwa na mduara wa mwanga wa kijani-kibichi, wenye tishu zilizolowa maji.
Kwa vile majani yaliyoambukizwa ndiyo chanzo kikuu cha vijimbegu vya kuvu, kuweka mfuko juu ya ndizi, mara tu baada ya kuvunwa, hutengeneza kizuizi cha kuzuia vijimbegu vya kuvu kuenea kwenye matunda. Uwekaji wa mafuta ya mwarobaini (1500 ppm) kwa kila mililita 5 na gramu 1 ya surf au sandovit (1ml) kwa lita moja ya maji yanaweza kutumika kwa kuzuia, katika hatua ya utokaji maua ya mazao na wakati wa kuonekana kwa mara ya kwanza.
Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kinga na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Kunyunyizia majani na matunda kwa maneb kila baada ya wiki 2 au mara moja kwa mwezi kwa mwaka mzima kunaweza kupunguza kuenea kwa vijimbegu vya kuvu. Kunyunyizia dawa za kuua kuvu kama vile folpet, chlorothalonil, mancozeb, triazoles, propiconazole na zile za familia ya strobilurins, kila wiki mbili kunaweza kutoa matokeo bora dhidi ya ugonjwa huo.
Dalili husababishwa na kuvu/fangasi aitwae Phyllosticta maculata. Kuvu hawa wanaweza kuathiri mimea ya migomba katika hatua zote za mzunguko wa uzalishaji na inachukuliwa kuwa kijimbegu/kiiniyoga chenye unyevu kwa kuwa vijimbegu/viiniyoga vya kuvu vinahitaji maji kama njia ya kutawanywa (matone ya mvua, michirizi ya maji, matone ya umande kwa mfano). Mabaka ya migomba pia yanaweza kuenezwa kupitia uhamishaji wa mimea na matunda yaliyoambukizwa. Madoa ya mabaka yana miundo ya kuvu ambao hutoa vijimbegu/viiniyoga. Vijimbegu hivi vinapoota, huzalisha nyuzi ambazo hupenya kwenye mimea inayohifadhi kuvu na kuongezeka ndani kwa ndani na kati ya seli, na kutengeneza madoa au vidonda vipya kwenye tabaka za juu za tishu za mmea. Kipindi cha kuatamia kinaweza kupungua hadi siku 20 katika hali ya hewa ya joto yenye unyevunyevu.