Mahindi

Doa Kawahia la Mahindi

Physoderma maydis

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa madogo yenye rangi ya njano hadi kahawia kwenye majani, shina(mabua), ala (mfuko-jani) wa shina, na kumvi( kapi/ganda la nafaka) za mahindi.
  • Sehemu za tishu zilizoathirika zinaweza kufunika sehemu kubwa ya jani.
  • Madoa ya kahawia hadi meusi kando ya mshipa mkuu wa jani au karibu sana na mshipa huo.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Mahindi

Dalili

Maambukizi husababisha madoa madogo yenye rangi ya njano hadi kahawia kwenye majani, shina(mabua), ala (mfuniko) wa shina, na kumvi za mahindi. Kadri ugonjwa unapoendelea, madoa nayo huongezeka ukubwa na kuwa mengi zaidi. Mabaka yanayotokea au sehemu ya tishu zilizoathirika vinaweza kufunika sehemu kubwa ya jani. Rangi yake kwa kawaida hutofautiana kutoka ya manjano hadi kahawia na hufanana na dalili zinazotokana na aina fulani za kutu. Hata hivyo, tofauti na magonjwa ya kutu, vidonda vya kuvu P. maydis (anayesababishwa ugonjwa Doa Kawahia la Mahindi) mara nyingi hujitokeza katika maeneo tofauti kwenye jani, hususani kwenye kikonyo chake. Tofauti nyingine ni kwamba madoa yenye rangi ya giza hadi meusi hujitokeza kwa uwazi kwenye au karibu na mshipa mkuu wa jani. Kwa aina ya mbegu zilizo kwenye hatari ya kuambukizwa, mshipa wa kati unaweza kufunikwa na vidonda hivi na unaweza kubadilika rangi kutoka ya chokoleti/kahawia nyekundu ya kahawia au zambarau.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hakuna matibabu ya kibaiolojia yanayopatikana dhidi ya kuvu wa Doa Kawahia la Mahindi. Tafadhali tujulishe ikiwa unafahamu uwepo wa tiba yoyote ya aina hiyo. Udhibiti wa kitamaduni unaolenga kutengeneza mazingira yasiyo muafaka kwa kuvu ndio mbinu muhimu zaidi ya kuepuka kutokea kwa ugonjwa huu na milipuko inayoweza kutokea.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zinazotumia kinga na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Hakuna matibabu ya kemikali yanayopendekezwa dhidi ya kuvu wanaosababisha ugonjwa huu kwa sababu ni ugonjwa unaotokea mara chache na athari zake kwenye mavuno zinapaswa kuwa ndogo.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na kuvu anayejulikana kitaalamu kama Physoderma maydis, kuvu ambao, wakati wa majira ya baridi huishi katika mabaki ya mazao yaliyoathiriwa au kwenye udongo hadi miaka 7 katika hali nzuri. Ugonjwa huu ni wa kawaida zaidi kwenye mashamba yanayolimwa mahindi kwa mfululizo au yenye mabaki mengi ya mazao, kwa mfano, pale ambapo mfumo wa kupunguza kiwango cha kulima hupungua. Maambukizi kwa kawaida huanza kwenye sehemu ya mmea ambayo maji hukusanyika baada ya mvua au umwagiliaji. Kutoka hapo, maambukizi/vimelea vya pili huenezwa kwa njia ya upepo au maji ya rasharasha kwenda sehemu zingine za mimea ambazo maji hukusanyika. Hii inaeleza ni kwa nini dalili hujitokeza zaidi kwenye sehemu za chini za majani ya zamani. Mwanga na joto ni mazingira muafaka yanayohitajika kuwezesha ugonjwa huo kuenea. Kwa ujumla, ugonjwa huu siyo hatari sana na una athari ndogo kwenye mavuno.


Hatua za Kuzuia

  • Fuatilia shamba mara kwa mara ili kugundua uwepo wa dalili za ugonjwa.
  • Fanya mzunguko mpana wa mazao, kwani kuvu/ukungu huishi kwenye mabaki ya mazao yaliyoathiriwa au kwenye udongo kwa miaka 2-7.
  • Ondoa mabaki ya mazao kwa kulima kwa kina au kuyachoma mbali na shamba.

Pakua Plantix