Tango

Chule ya Tango

Glomerella lagenarium

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa ya mviringo yenye rangi ya njano yenye unyevunyevu kwenye majani.
  • Madoa ya mviringo, meusi, yaliyozama kwenye matunda.
  • Utokaji wa magome na kunyauka kwa mashina.

Inaweza pia kupatikana kwenye

4 Mazao
Tango
Tikiti
Boga
Boga dogo (Zucchini)

Tango

Dalili

Dalili kwenye majani huanza kama vidonda vilivyotota maji ambavyo baadaye vinakuwa madoa ya mviringo yenye rangi ya manjano. Sifa kuu ya madoa haya ni kutokuwa ya kawaida na hubadilika rangi na kuwa ya kahawia au meusi kadri yanavyoongezeka ukubwa. Vidonda kwenye mashina pia vinaonekana, na kadri vinavyoongezeka ukubwa, vidonda hivi huondoa tishu za mishipa kuzunguka shina na hivyo kusababisha mashina na mmea unaotambaa kunyauka. Kwenye matunda, madoa makubwa ya mviringo, meusi na yaliyozama hujitokeza, na baadaye kuwa vikwachu (vidonda vikubwa). Kwenye tikiti maji, madoa yanaweza kuwa na kipenyo cha milimita 6-13 na kina cha hadi milimita 6. Kunapokuwa na unyevu, sehemu ya kati nyeusi ya kidonda/jereha inafunikwa na mkusanyiko wa viiniyoga (vijimbegu vya kuvu) vyenye rangirangi. Vidonda kama hivyo pia hutokea kwenye matango na tikiti tamu( muskmeloni). Vikwachu vyenye rangi mithili ya pinki ni dalili kuu ya ugonjwa huu kwenye mazao jamii ya maboga (kama vile maboga, matango, matikiti, n.k).

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Mchanganyiko wa shaba ulioidhinishwa kwa kilimo hai zinaweza kupuliziwa dhidi ya ugonjwa huu kwenye mazao ya jamii ya maboga na zimeonyesha matokeo mazuri hapo awali. Mchanganyiko wenye viumbe hai wa udhibiti wa kibaiolojia kama vile bacteria aina ya Bacillus subtilis pia unapatikana.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zinazotumia hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia, ikiwa yanapatikana. Tumia dawa za kuua kuvu zilizothibitishwa kwa vipindi vya kawaida, na mara nyingi zaidi ikiwa mvua zinanyesha mara kwa mara. Tumia dawa za kuua kuvu zenye chlorothalonil, maneb, na mancozeb. Mchanganyiko wa chlorothalonil na mancozeb umeonekana kuwa na ufanisi mkubwa unapotumiwa kama dawa ya kupuliza kwenye majani.

Ni nini kilisababisha?

Dalili kwenye majani na matunda husababishwa na kuvu/fangasi anayefahamika kitaalamu kama Glomerella lagenarium, ambae huishi msimu wote wa baridi kwenye masalia ya mazao yenye magonjwa kutoka msimu uliopita au inaweza kuenezwa kupitia mbegu za mimea jamii ya maboga. Wakati wa majira ya kuchipua, wakati hali ya hewa inapokuwa na unyevunyevu zaidi, kuvu huachilia vijimbegu vya kuvu(viiniyoga) vinavyoenezwa kwa njia ya hewa ambavyo huambukiza mmea wa matango na majani yaliyo karibu na udongo. Mzunguko wa maisha ya kuvu hutegemea sana unyevunyevu wa mazingira, unyevunyevu wa majani, na joto la juu kidogo, ambapo 24°C inachukuliwa kuwa ndio kiwango muafaka kwa mzunguko wa maisha ya kuvu. Vijimbegu vya kuvu havimei kwenye joto la chini ya 4.4°C au juu ya 30°C au ikiwa havipati utando wa unyevunyevu. Zaidi ya hayo, vimelea vinahitaji maji ili kuachia vijimbegu vya kuvu kutoka kwenye ganda lao lenye kunata kwenye mwili wa matunda. Hii inafafanua ni kwa nini chule ya matango mara nyingi hujitokeza katikati ya msimu baada ya mimea kutoa majani mengi.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu zilizothibitishwa na zisizo na magonjwa.
  • Chagua aina ya mbegu zenye uwezo wa kuhimili magonjwa, ikiwa zinapatikana katika eneo lako (aina kadhaa zinapatikana kwenye maduka).
  • Epuka usogezaji wa vifaa vya kilimo au wafanyakazi shambani wakati majani yakiwa na unyevunyevu.
  • Ikiwa ni lazima kutumia umwagiliaji wa juu, fanya umwagiliaji huo mapema asubuhi na hakikisha majani yamekauka kabla ya kuingia usiku.
  • Fanya mzunguko wa mazao kati ya matango na mazao mengine yasiyo jamii yake (kama vile maboga na matikiti maji) kwa mzunguko wa miaka mitatu mitatu.
  • Fanya usafi mzuri wa shamba kwa kulima chini ya matunda na mmea unaotambaa mwishoni mwa kila msimu.

Pakua Plantix