Soya

Ubwiri Unga wa Soya

Erysiphe diffusa

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Mwanzo, ukungu mweupe wa unga kwenye sehemu ya juu ya jani, baadaye hukua na kufunika uso wa juu na wa chini wa jani.
  • Inaweza pia kukua kwenye maganda na mashina.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Soya

Dalili

Ubwiri unga huonekana kwa mara ya kwanza kama sehemu ndogo za duara za ukungu mweupe na unga kwenye sehemu ya juu ya jani la soya. Maeneo yaliyoambukizwa huongezeka na kufunika sehemu kubwa ya jani, ikiwa ni pamoja na nyuso za juu na za chini. Ukuaji wa ukungu unaweza pia kuonekana kwenye shina na maganda ya tunda. Wakati wa maambukizi makali, sehemu zote za mmea wa soya hufunikwa na ukungu wa unga mweupe hadi kijivu nyepesi. Baadhi ya aina za soya zinaweza kuonyesha klorosisi au njano ya majani na mabaka ya kutu kwenye upande wa chini wa majani. Mimea iliyoathiriwa sana inaweza kuangusha/kupukutisha majani mapema. Maganda ya soya yaliyo ambukizwa sana kwa kawaida huwa na mbegu za kijani zilizonyauka, ambazo hazijastawi, zilizoharibika na bapa.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Kwa maeneo madogo ya shamba, mchanganyiko wa maji na maziwa unaweza kufanya kazi kama dawa ya asili ya kuua kuvu. Nyunyiza mchanganyiko huo kwenye majani kila baada ya siku ya pili. Vitunguu swaumu vilivyochanganywa na maji au sodiamu baikaboneti(soda ya kuoka) iliyo changanywa na maji pia vinaweza kuleta matokeo ya kuridhisha. Kunyunyizia salfa iliyo lowanishwa kwa 3g/lita ya maji pia kunafaa.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua kuvu zenye salfa inayoweza kulowanishwa, triflumizole, myclobutanil zinaonekana kudhibiti ukuaji wa kuvu/fangasi katika baadhi ya mazao.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na kuvu/fangasi aina ya Erysiphe diffusa, ambao vijimbegu/chavua zake hutawanywa hasa kwenye tishu za mmea zenye afya kwa upepo. Zinapoota na kupenya kwenye tishu, chavua hizi huunda mirija ya vijidudu na kujishikiza kwenye seli za majani kupitia mfumo wa kujishikilia. Hatimaye, hii huunda mifumo ya chakula na ukuaji unaoendelea na kupitiliza kwenye ngozi ya juu ya jani la soya (utando mweupe). Vijimbegu vinavyopeperushwa na upepo huanza maambukizi mapya na kurudia mzunguko wa ugonjwa hadi mimea ya soya inapo komaa. Ukuaji wa ugonjwa hutokea katika joto zaidi ya 30 ° C na hupendelea joto la kati. Mvua haionekani kusababisha ugonjwa huu. Ingawa mimea ya soya huathirika katika hatua yoyote ya ukuaji, lakini dalili ni nadra kabla ya katikati hadi mwishoni mwa msimu wa hatua za uzalishaji.


Hatua za Kuzuia

  • Panda mimea kukiwa na nafasi ya kutosha kati ya mmea na mmea ili kuruhusu uingizaji mzuri wa hewa.
  • Chagua aina za mbegu au mimea iliyo sugu au inayostahimili magonjwa kwa jili ya kupanda.
  • Fuatilia au kagua shamba mara kwa mara kujua dalili za ugonjwa.
  • Ondoa majani yaliyoambukizwa mara tu madoa ya kwanza yanapo onekana.
  • Usiguse mimea yenye afya baada ya kugusa mimea iliyoambukizwa.
  • Kulima baada ya kuvuna na kabla ya kupanda kunaweza kusaidia kuvunja mabaki ya mazao na kuharibu vimelea vya magonjwa.

Pakua Plantix