Botryotinia squamosa
Kuvu
Maambukizi yanaweza kutokea katika hatua yoyote ya ukuaji na kawaida hutokea kwanza kwenye majani makongwe. Dalili za awali huonekana ndogo (1-5 mm), madoa meupe ya duara au marefu kwenye sehemu ya juu ya jani. Madoa yaliyo jitenga na baadae kuwa makundi ya madoa yaliyozungukwa na duara angavu la kijani mpauko au la rangi ya fedha ambalo mara nyingi huwa na mwonekano uliotota maji mwanzoni. Baada ya muda, idadi ya vidonda huongezeka na katikati ya madoa ya zamani huzama na kuwa na rangi ya majani makavu, ishara ya kuendelea kufa kwa tishu/seli. Sifa ya mpasuko ambao umekaa kwa urefu kwenye kidonda unaweza kuonekana katika hatua za baadaye. Ncha za majani na kingo hulainika na taratibu huwa na seli zilizokufa, na kusababisha kutengeneza mabaka na kufa. Katika hali nzuri, ugonjwa pia huathiri kitunguu chenyewe, kupunguza ukubwa wake na ubora wake. Ugonjwa unapoenea zaidi, madoa makubwa ya manjano ya mimea inayokufa yanaweza kuonekana kwa mbali ukiwa shambani.
Hakuna matibabu ya kibayolojia yanayoonekana kupatikana kwa sasa kutibu ugonjwa huu. Wasiliana nasi ikiwa unajua mojawapo.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Utamaduni mzuri ni muhimu ili kupunguza hatari ya kuambukizwa. Iwapo dawa za kuua kuvu zinahitajika, bidhaa zilizo na iprodione, pyrimethanil, fluazinam au cyprodinil pamoja na fludioxonil hutoa matokeo bora zaidi zinapotumiwa kwa kunyunyizia. Bidhaa zingine zenye chlorthalonil na mancozeb pia hufanya kazi lakini zina ufanisi mdogo. Uwekaji wa dawa za kuua kuvu kwa ufukizaji wa ardhini unaweza kuwa na ufanisi zaidi kuliko njia za kunyunyizia kwa juu.
Ugonjwa huu husababishwa na fangasi aitwae Botrytis squamosa, ambae huishi kwenye vitunguu vilivyoambukizwa au uchafu mwingine wa mimea ulioachwa shambani, au kwenye maghala ya kuhifadhia. Ikiwa hali ya hewa ni rafiki, vijimbegu vya kuvu huzalishwa kwenye tishu hizi na kusambazwa na upepo kwenye mimea ya karibu, ambayo hutumika kama chanzo kikuu cha maambukizi. Halijoto kati ya 10 na 20 °C, mvua nyingi, vipindi virefu vya unyevu kwenye majani au unyevu mwingi husaidia mzunguko wa maisha ya kuvu. Dalili zinaweza kufanana na magonjwa mengine au matatizo kama vile mfadhaiko wa ukame, majeraha ya mvua ya mawe, mashambulizi ya vithiripi au uharibifu unao tokana na dawa za kuua magugu.