Erysiphe necator
Kuvu
Ukubwa wa dalili hutegemea aina ya mzabibu na hali ya mazingira. Kwa kawaida, madoa ya yenye rangi ya manjano (ya kipenyo cha mm 2 hadi 10) huonekana kwanza kwenye upande wa juu wa majani machanga, mara nyingi karibu na kingo. Ukuaji wa kuvu walio mithili ya majivu hadi unga (poda) mweupe huongezeka polepole kwenye madoa haya. Kadiri ugonjwa unavyoendelea, madoa huongezeka ukubwa na yanaweza kuungana na kufunika jani zima, ambapo mwishowe jani linaweza kupinda, kukauka na kudondoka. Sehemu za mishipa upande wa chini wa majani yaliyoathirika zinaweza kugeuka na kuwa na rangi ya kahawia. Kwenye vishina, mabaka yaliyotawanyika yenye rangi ya kahawia au nyeusi pia huonekana. Katika hatua za baadaye, maua na zabibu pia huathirika, na mizabibu hutoa harufu ya kuvu. Zabibu zilizoathirika zinaweza kubadilika na kuwa za rangi ya kahawia iliyokoza na zenye makovu au kukauka. Kwa baadhi ya aina za mizabibu, ueneaji wa kuvu unakuwa mdogo na dalili zinaishia kwa majani kubadilika rangi na kuwa ya kijivu au zambarau.
Salfa, dawa za kuua wadudu zinazotokana na mazao ya bustani, na aina mbalimbali za dawa za kibiashara zinakubalika kwa mizabibu iliyoidhinishwa kwa kilimo hai. Vijidudu/Vimelea vya kuvu aina ya Ampelomyces quisqualis, vimeripotiwa kuwa na uwezo wa kuvuruga mzunguko wa maisha ya vimelea vinavyosababisha ugonjwa wa ubwiri unga. Utitiri wanaokula kuvu na mbawakawa, wote hao wameripotiwa kupunguza makundi ya ubwiri ungakwenye baadhi ya mizabibu.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye njia za kukinga pamoja na tiba za kibaiolojia ikiwa zinapatikana. Upuliziaji mzuri wa dawa kwenye sehemu zote za kijani za mmea na upuliziaji kwa wakati sahihi ni jambo muhimu katika kudhibiti ubwiri unga. Dawa za kukinga zinazotokana na salfa, mafuta, bikabonati, au asidi ya mafuta vinaweza kutumika kupunguza maambukizi ya awali. Bidhaa za madawa zinazotokana na strobilurins na azonaphthalenes zinaweza kupuliziwa mara baada ya ubwiri unga unapogunduliwa.
Ugonjwa wa ubwiri unga husababishwa na vimelea vya kuvu (ukungu/fangasi) aina ya Erysiphe necator. Kuvu hawa huishi msimu wote wa baridi kama viiniyoga (vijimbegu) vilivyolala kwenye machipukizi yaliyosimama kwa muda kukua au kwenye mipasuko ya magamba ya miti. Katika majira ya kuchipua, viiniyoga (vijimbegu) hivi vya kuvu hubebwa na upepo kwenda kwenye mimea mipya (na hivyo kusababisha maambukizi ya awali). Baada ya ubwiri kuenea kwenye sehemu mbalimbali za mmea, huanza kuzalisha viiniyoga vipya vya kuvu ambavyo vinasambazwa zaidi na upepo (maambukizi ya pili). Unyevunyevu huru (yaani unaotokana na umande, ukungu, na mvua), uwepo wa majimaji kwenye majani kwa muda mrefu au hali ya hewa yenye mawingu; yote hayo ni mazingira rafiki kwa uzalishaji wa viiniyoga wa kuvu lakini si lazima kwamba yawezesha mchakato wa maambukizi (tofauti na magonjwa mengine ya ukungu/kuvu). Mzunguko wa maisha ya kuvu pia unawezeshwa vizuri na mnururisho wa chini hadi wa wastani pamoja na joto linaloanzia nyuzi joto 6 °C hadi 33 °C (kiwango kinachofaa zaidi ni 22 °C hadi 28 °C). Ubwiri unga unapungua kwenye sehemu za majani zilizowekwa wazi kwenye na joto zaidi ya 35 °C, mwanga wa moja kwa moja wa jua, na mvua ya mara kwa mara.