Canola

Uozo Shina

Plenodomus lingam

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Vidonda vyote vya duara, vya kijivu iliyopauka vikiwa na vitone vya vidoa vyeusi na tishu nyeusi zilizokufa hutokea kwenye majani.
  • Aina zote za vidonda zimezungukwa na maduara ya mwanga wa njano.
  • Mashina huonyesha vidonda vya rangi ya kijivu ambavyo vinaweza kukua na kuwa vikwachu.
  • Vinapokua, vikwachu (vidonda vya mmea) huondoa magome kuzunguka shina na kulidhoofisha, na hivyo kusababisha kuanguka na kufa kwa mmea.

Inaweza pia kupatikana kwenye

3 Mazao
Kabichi
Canola
Koliflawa

Canola

Dalili

Ukali wa dalili hutofautiana sana kutegemea na mazao au aina inayohusika, kimelea chenyewe, na hali ya mazingira iliyopo. Katika hali yoyote, dalili kuu zinaonekana kwenye majani na shina. Vidonda vya majani vinajumuisha vidonda vyote vya duara, kijivu iliyopauka vikiwa na vitone vya vidoa vyeusi na tishu nyeusi zilizokufa. Rangi ya manjano ya mshipa wa jani au ya mabaka yote kuzunguka vidonda pia ni ya kawaida (mduara wa mwanga wa njano). Mashina pia huonyesha vidonda vya kijivu vinavyoweza kuwa vidogo, vya umbo la mstatili, vya kahawia hadi vile vinavyozunguka shina lote. Madoa madogo yenye weusi yanaweza pia kuonekana kwenye shina. Vinapokua, vikwachu (vidonda) huondoa magome kuzunguka shina na kulidhoofisha, na hivyo kusababisha matunda kuiva mapema, kuanguka na kufa kwa mmea. Maganda yanaweza kuonyesha dalili katika umbo la vidonda vya kahawia vyenye kingo nyeusi, vinavyosababisha kuiva mapema na maambukizi ya mbegu.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hakuna hatua za udhibiti wa kibaolojia zinazoweza kupatikana ili kupambana na magonjwa haya. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unafahamu yoyote.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua kuvu huwa na athari ndogo sana pindi kuvu inapofika kwenye shina na matibabu yanaweza tu kupendekezwa kwenye mashamba ambayo mavuno mengi yanatarajiwa. Prothioconazole inaweza kutumika kama dawa ya kunyunyuzia majani. Tiba amilifu ya mbegu kwa kutumia prochloraz iliyoongezwa kwenye thiram inaweza kupunguza maambukizi ya miche yanayosababishwa na maambukizi ya kuvu wa udongo aina ya Phoma anaesambazwa kwa njia mbegu.

Ni nini kilisababisha?

Uozo Shina (pia inajulikana kama Kuvu wa Vikwachu/vidonda vya shina) kwa kweli husababishwa na aina mbili za kuvu/fangasi, ambazo ni Leptosphaeria maculans na L. biglobosa. Kuvu hawa wanaishi kwenye mbegu msimu wote wa baridi, au kwenye mabaki ya mazao na mashina ambayo yanabaki shambani. Wanaanza kuzalisha vijimbegu wakati wa mwanzo wa hali ya hewa ya joto na unyevunyevu katika majira ya kuchipua. Vijimbegu hivi husambazwa na upepo au matone ya mvua hadi sehemu zenye afya za mmea, hususani kwenye majani ya chini na kitako cha shina. Kuota kwa vijimbegu na ukuaji wa kuvu kwenye tishu za mmea huchochea kutokea kwa dalili. Ikiwa kotiledoni (majani mbegu) zinapata maambukizi, miche inaweza kufa mapema kwenye msimu (ugonjwa kiuno). Kuvu huenea kutoka majani machanga hadi kwenye shina, ambapo inakua na kuunda vidonda kwenye muunganiko kati ya kikonyo na shina au kuzunguka taji la mmea. Hii inapunguza usafirishaji wa maji na virutubisho kupitia shina, na kifo na kuanguka kunaweza kutokea. Ni ugonjwa maarufu kwa mmea wa rapeseed (jamii ya kabichi) na mazao mengine ya familia ya Brassica (canola, tanipu, brokoli, Kabichi vifundo, kabichi).


Hatua za Kuzuia

  • Hatua muhimu zaidi dhidi ya ugonjwa huu ni kutumia aina za kanola zinazostahimili magonjwa.
  • Panga mzunguko wa mazao kwa kutumia mimea isiyohifadhi vimelea vya magonjwa.
  • Lima na fukia/zika mabaki ya mazao baada ya mavuno.
  • Ulimaji wa juu juu unaweza kuzuia kuvu kufikia majani ya chini na mashina.

Pakua Plantix