Komamanga

Chule ya komamanga

Glomerella cingulata

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa meusi yenye mduara angavu (halo) wa njano.
  • Madoa kwenye jani zima katika hatua ya baadaye.
  • Kudondosha majani mapema.
  • Matunda makavu, kahawia hadi meusi.
  • Maganda ya mbegu huoza.
  • Uvimbe/vikwachu kwenye matawi.
  • Mizizi huingiliana na kuzunguka shina na kusababisha mmea kufa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Komamanga

Dalili

Kuvu husababisha dalili mbalimbali, kulingana na tishu zilizoshambuliwa na hali ya hewa. Madoa madogo sana yaliyozama ya rangi mbalimbali huonekana kwenye majani, shina, maua au matunda, mara nyingi yakiwa yamezungukwa na mduara angavu wa njano wenye alama zaidi au kiasi. Kwenye majani, madoa huongezeka baadaye na kuunda vidonda na yanaweza kufunika sehemu kubwa ya ubapa wa jani. Yanageuka njano na yanaweza kuanguka mapema na kusababisha kupukutika kwa majani. Madoa kwenye matunda yana rangi ya kahawia hadi kahawia iliyokolea, kwanza ni ya mviringo, kisha yanakuwa hayana umbo maalumu kadri yanavyopanuka. Tunda hilo baadaye hulainika na kuoza hutokea kwenye arili ambazo hubadilika kuwa kijivu iliyokolea au nyeusi lakini hazina maji. Chule pia inaweza kushambulia vijitawi na matawi na kusababisha uvimbe/vikwachu, ambayo ni maeneo ya tishu zilizozama, zilizoambukizwa na kingo zilizovimba. Maambukizi ya shina mara chache yanaweza kusababisha mguguno unao kwamisha maji navirutubisho visipite na kufa

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Mawakala wa udhibiti wa kibayolojia wanaojulikana ni fangasi washindani Aspergillus flavus, Hypocrea rufa, Hyponectria tuberculariformis, na Nectriella muelleri. Wa kwanza tu ndiye mpinzani wa kweli. Wengine ni wanyonyaji au vimelea wa magonjwa.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa ya kwanza ya kuzuia inaweza kunyunyiziwa wakati maua yanaanza na hali za kimazingira zikiwa nzuri kwa kuvu. Kisha nyunyiza kwa muda wa siku 15 mara mbili, ikiwa ni lazima. Viambata hai vinavyotumika ni propiconazole, mancozeb au mchanganyiko wa mancozeb na tricyclazole. Nyunyiza dawa za kuua kuvu tu zenye usajili halisi kwajili ya komamanga. Ni muhimu kufuata viwango vilivyoainishwa na kutumia dawa za kuua kuvu zenye muundo tofauti wa ufanyaji kazi ili kuzuia ukinzani/usugu.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na fangasi Glomerella cingulata. Huishi katika mabaki ya mimea iliyoambukizwa kwenye uso wa udongo au katika matunda yaliyokaushwa. Katika majira ya kuchipua, vijimbegu vyake huenezwa kupitia mvua au upepo na huambukiza matawi au mimea ya jirani. Hatua zinazoathirika zaidi ni kipindi cha maua na ukuaji wa matunda. Majeraha kutokana na miiba ya miti, wadudu, na wanyama huchochea mchakato wa kuambukizwa. Mvua za mara kwa mara, unyevu mwingi (50-80%) na kiwango cha joto cha 25-30°C ni rafiki kwa mzunguko wa maisha ya kuvu. Hata hivyo, kwa kawaida kuvu huwa bwete katika msimu wa kiangazi. Hata madhara ya mwanga yanaweza kusababisha uharibifu wa uzuri/mvuto wa matunda na kufupisha mda wake wa kuhifadhi. Mimea mingine inashoshambuliwa ni kwa mfano Maembe, Mapera na Papai.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mimea yenye afya kutoka kwenye vyanzo vilivyoidhinishwa.
  • Tumia aina zinazostahimili zinazopatikana katika eneo lako.
  • Weka nafasi ya kutosha kati ya mimea ili kuhakikisha uingizaji hewa mzuri.
  • Weka mifereji ya maji vizuri kwenye shamba na usitumie umwagiliaji wa juu.
  • Weka mbolea baada ya majani kufunguka na mvua ya masika kukoma.
  • Rutubisha mazao yako vizuri ili kuepuka athari kwenye mavuno.
  • Hakikisha usafi wa shamba, kwa kudhibiti magugu kwa mfano.
  • Epuka uharibifu wa mitambo au kimaumbile kwenye mmea.
  • Angalia mimea au shamba lako kwa dalili zozote za ugonjwa, hasa wakati wa maua na ukuaji wa matunda.
  • Pogoa wakati wa majira ya baridi na takasa zana za kupogolea.
  • Kusanya na uondoe majani yaliyoanguka na vijitawi na matawi yaliyoambukizwa wakati wa msimu wa ukuaji na katika vuli.

Pakua Plantix