Pseudocercospora punicae
Kuvu
Dalili zinaweza kuzingatiwa kwanza kwenye sepali za maua. Madoa madogo ya mviringo na kahawia hadi meusi huonekana hapo. Madoa baadaye hukua, kuungana na kugeuka kuwa meusi zaidi. Umbo linakuwa isivyo kawaida na madoa yanaweza kufikia ukubwa wa 1 hadi 12 mm kwa kipenyo. Kwenye matunda, madoa hufanana na vidonda vinavyoonekana kukiwa na baka la bakteria lakini ni meusi zaidi, tofauti, ya ukubwa mbalimbali, bila nyufa na hakuna kunata. Kwenye majani, madoa yametawanyika, mviringo au yasiyo umbo maalumu, rangi nyekundu iliyokolea inayokaribia nyeusi na ukingo wa manjano ulioenea. Madoa huanzia 0.5 hadi 5 mm kwa kipenyo na hayaunganishwi. Majani yenye madoadoa huwa ya kijani hafifu, yanageuka manjano na kuanguka. Madoa meusi ya duaradufu yanaonekana kwenye vijitawi, huwa bapa na kubonyea yenye ukingo ulioinuka. Vijitawi vilivyoambukizwa hukauka na kufa.
Samahani, hatujaweza kupata chochote kuhusu mawakala wa udhibiti wa kibayolojia wa ugonjwa huu. Tunatazamia kujaza pengo hili.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ikiwa kizingiti cha kiuchumi kinafikiwa, hatua za udhibiti zinapaswa kuanzishwa. Kunyunyizia dawa mbili hadi tatu kwa muda wa siku 15 baada ya kutokea kwa matunda kunatoa udhibiti mzuri wa ugonjwa. Viambata hai vinavyotumika ni mancozeb, conazole, au kitazin. Nyunyiza dawa za kuua kuvu tu zenye usajili halisi wa kutumika kwajili ya komamanga. Ni muhimu kufuata viwango vilivyoainishwa na kutumia dawa za kuua kuvu zenye mfumo tofauti wa ufanyaji kazi ili kuzuia ukinzani/usugu. Kuheshimu muda wa kusubiri pia ni muhimu sana.
Dalili husababishwa na fangasi Pseudocercospora punicae. Anaweza kuishi katika uchafu wa mimea na katika sehemu za shina zilizoambukizwa za mmea. Anaenezwa na vijimbegu vinavyopeperushwa na upepo. Kuibuka kwa ugonjwa huchochewa na mvua na udongo uliojaa maji. Hivyo mchakato wa maambukizi na kuenea kwa ugonjwa ni haraka wakati wa hali ya unyevu na mvua. Madoa ya majani yanaweza kupunguza mavuno kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Yanapunguza eneo ambalo linaweza kutoa nishati kupitia usanisinuru. Majani yaliyoambukizwa hayawezi kuuzwa kwa uzalishaji wa chai au kitu kingine chochote. Madoa ya matunda husababisha hasara ya kiuchumi ya bidhaa inayouzwa. Matunda yaliyoambukizwa hayawezi kuuzika pia.