Pectobacterium carotovorum
Bakteria
Dalili za awali katika machipukizi yaliyopandwa karibuni huonekana kama kuoza kwa tishu za ndani ya mashina-bandia na mizizi. Hii inajiainisha kwa uwepo wa maeneo ya kahawia nyeusi au manjano yaliyolowana maji kwenye tishu za ndani na harufu mbaya. Wakati mimea iliyoathiriwa inapokatwa wazi kwenye eneo la kola, mtiririko wa manjano hadi nyekundu huonekana. Kuoza kwa eneo la kola hufuatiwa na majani kuwa na afya duni ghafla, ambapo baadaye hukauka kabisa. Katika hatua za baadaye za ugonjwa huo, kitako cha shina huvimba na kupasuka. Katika mimea yenye umri mkubwa, kuoza hutokea kwenye eneo la kola na pia sehemu za chini (vitako) za majani. Ikiwa mimea iliyoathiriwa inavutwa, huvunjika kwenye eneo la kola na kuacha balbu na mizizi kwenye udongo. Mlipuko wa ugonjwa huu mara nyingi huonekana miezi 3-5 baada ya kupanda.
Hakuna matibabu ya kibayolojia ambayo yamepatikana hadi sasa kutibu ugonjwa huu. Mara baada ya ugonjwa huo kugunduliwa hakuna uwezekano wa kuponya mimea iliyoambukizwa au kupunguza maambukizi. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua matibabu yoyote ya kibaolojia.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Mara baada ya ugonjwa huo kugunduliwa hakuna uwezekano wa kuponya mimea iliyoambukizwa au kupunguza maambukizi. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua matibabu yoyote ya ugonjwa huu kwa madawa.
Ugonjwa huu husababishwa na spishi ndogo ya bakteria aitwae Pectobacterium carotovorum inayoenezwa na udongo. Bakteria hawa huishi kwenye udongo wenye unyevunyevu na na mabaki ya mazao. Huenezwa kati ya miti kupitia mvua na maji ya umwagiliaji lakini pia kwa kupanda mimea iliyoambukizwa. Hususani mimea michanga (machipukizi ya mizizi) huathiriwa na ugonjwa huo. Vimelea vya magonjwa huingia kwenye mfumo wa mizizi kupitia majeraha ya asili na yasiyo ya asili kwenye tishu za mmea. Dalili hizi hutokana na kuoza kwa tishu za ndani za shina na uharibifu wa usafirishaji maji na virutubisho. Unyevu mwingi na mvua za mara kwa mara husaidia ukuaji wa bakteria. Maambukizi huwa ni mabaya zaidi katika kipindi cha hali ya hewa ya joto na majimaji wakati wa majira ya joto. Hasara za kiuchumi ni kubwa zaidi endapo ugonjwa huu unatokea wakati wa kutokea kwa mikungu.