Pezizomycotina
Kuvu
Ugonjwa wa masizi unaweza kupatikana kwenye miti ya miembe na mimea mingine yoyote ambayo awali ililiwa na wadudu. Ukungu hukua kwenye ute wa asali, ambao ni ute mzito na wenye sukari unaozalishwa na baadhi ya wadudu ili kuvutia wadudu wenzao. Kutumia ute wa asali kama chanzo cha chakula, hatua kwa hatua kuvu hufunika sehemu iliyoathirika ya mmea, na kuifanya iwe na rangi ya vivuli mbalimbali vyeusi. Ugonjwa wa masizi sio vijidudu na sio vimelea vya magonjwa ya kuvu, na kwa hivyo haukai kwenye tishu za mimea au kusababisha dalili. Hata hivyo, hubadilisha uwezo wa mmea kufanya usanisinuru na kubadilishana gesi na anga. Majani yaliyoathirika sana yanaweza kufa na kuanguka, hivyo kuathiri ukuaji na uhai wa mimea.
Tumia mchanganyiko wa mafuta ya mwarobaini, ambayo ni kiungo cha asili chenye wigo mpana, ili kuzuia nzi weupe, vidukari, vidugamba, mchwa, na vidukari-sufu/vidung'ata. Mafuta ya mwarobaini pia hupunguza ukuaji wa kuvu yenyewe. Sabuni ya kuua wadudu au sabuni ya vyombo (kwa mfano, kijiko kimoja cha chakula kwa lita 5 za maji) inaweza kunyunyiziwa kwenye mimea iliyoathirika. Baada ya kuruhusu mchanganyiko wa sabuni kukaa kwenye mimea, unaweza kuoshwa, na hivyo kuondoa ukungu.
Daima fikiria mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Viuatilifu vya kiwandani vya familia ya organophosphate vinaweza kutumika kuzuia wadudu kula kwenye mmea.
Wadudu wanaonyonya floemu kama vile panzijani (Amritodus atkinsoni), nzi weupe, vidukari, na wengine wengi wanahusishwa na ugonjwa huu kadri wanapokula kwenye utomvu wa mimea. Katika mchakato wa kula, ute wa asali hutolewa juu ya uso wa mmea, hivyo kuunda mazingira bora kwa ukuaji wa ukungu wa masizi (ugonjwa wa masizi). Ute wa asali unaweza kudondoka kwenye majani au mimea iliyo jirani, na hivyo kueneza kuvu zaidi. Kuvu huishi kama ukungu au kama vijimbegu kwenye sehemu za mimea, zana, au vyombo vya usafirishaji. Wadudu pia hueneza ukungu kutoka mmea mmoja hadi mwingine. chungu/sisimizi, kwa mfano, huwa wanalinda maeneo yaliyokaliwa na ukungu wa masizi kwa manufaa yao wenyewe.