Neofabraea malicorticis
Kuvu
Dalili ya kawaida ya maambukizi ya chule au kuvu kwenye miti ya matunda ni kuonekana kwa vikwachu (vidonda vya mti) kwenye vitawi vichanga na matawi. Katika hatua za mwanzo, sifa zake ni ukuaji wa madoa madogo ya mviringo, yenye rangi nyekundu hadi zambarau na kunapokuwa na unyevu. Kadri madoa yanapokua, hatimae yanarefuka kidogo na kuzama, na rangi kuwa ya chungwa hadi kahawia. Kadri gome linapoharibika, nyufa hukua kwenye kingo na kuanza kujikunja kuelekea juu. Ukuaji wa kuvu au ukungu mweupe unaweza kuonekana katikati yao. Vitawi vichanga vinaweza kuzungukwa na vikwachu au vidonda vya mti na hatimae vitawi hivyo kufa. Majani machanga au matunda pia yanaweza kuathiriwa na kuwa na madoa pamoja na mabaka ya kahawia, ambayo kwa suala la matunda, husababisha uozaji unaofanana na jicho la ng'ombe wakati wa kuyahifadhi. Hususani kwa aina zinazoweza kuathirika kwa urahisi, inaweza kusababisha mti kupukutika majani na kupunguza uimara wake. Hatua hiyo hatimae husababisha kupungua kwa ubora wa matunda.
Uwekaji wa mchanganyiko wa Bordeaux au salfa ya shaba baada ya kuvuna kunaweza kupunguza matukio ya chule katika msimu unaofuata. Michanganyiko hii pia inaweza kutumika kabla ya mavuno ili kudhibiti uozaji unaofanana na jicho la ng'ombe kwenye matunda.
Wakati wote zingatia matumizi ya mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Hakuna dawa za kuua kuvu (fangasi) iliyothibitika kuwa na ufanisi wa kutokomeza kabisa vikwachu. Hata hivyo, matumizi ya dawa za kuzuia kuvu kabla ya kuvuna inaweza kupunguza matukio ya uozaji unaofanana na jicho la ng'ombe kwenye matunda wakati wa kuhifadhi. Utumiaji sawa wa dawa ya kuzuia kuvu baada ya kuvuna inaweza kupunguza vijidudu vya magonjwa kwa msimu unaofuata. Bidhaa zinazotokana na dawa za kuzuia ukungu kama vile kaptani, mankozeb au ziram zinaweza kutumika kwa madhumuni haya.
Dalili hizo husababishwa zaidi na ukungu (kuvu), yaani fangasi wanaoitwa Neofabra malicorticis, lakini fangasi wengine wanaotokana na familia moja wanaweza pia kuhusika. Fangasi hawa wanaweza kuishi kwenye mabaki ya mimea iliyoambukizwa au kwenye udongo. Wanakuwa na kustawi katika hali ya unyevu na joto, na mvua za mara kwa mara. Wakati wa majira ya kuchipua, huanza tena ukuaji na kuanza kutoa vijidudu vya viiniyoga (vijimbegu). Viiniyoga hivi hatimae huenezwa kwa urahisi kupitia maji ya umwagiliaji au mvua kwenye miti au mimea mingine. Baada ya hapo, vijidudu vya viiniyoga vinaweza kuingia kwenye miti kupitia majeraha madogo ya miti husika lakini pia vinaweza kupenya kwenye gome lisilo na majeraha. Vikwachu (yaani vidonda vya mti) hukua kwa mwaka 1 tu lakini kuvu (ukungu) huendelea kutoa idadi kubwa ya viiniyoga katika miaka 2 hadi 3 zaidi. Mimea au vitu mbadala vinavyoweza kubeba magonjwa ni pamoja na matunda aina ya komamanga na matunda mawe na vile vile matunda ya hawthorn na mountain ash. Aina zote za matufaha zinaathirika kirahisi na ugonjwa huu, kwa viwango tofauti. Miti ya mapeasi inaweza pia kuathirika na ugonjwa huu.