Karanga

Bakajani Alternaria la Karanga

Alternaria sp.

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa madogo ya kahawia yenye mduara angavu wa njano.
  • Vidonda vinaenea hadi kwenye mshipa wa katikati wa jani.
  • Majani kujikunja kuelekea ndani na kukakamaa.
  • Majani kuwa ya jano na kukauka.
  • Upukutishaji wa majani.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Karanga

Dalili

A. arachidis hutengeneza madoa madogo ya kahawia, yasiyo na umbo maalumu yaliyozungukwa na duara angavu la njano kwenye majani (madoa ya majani). A. tenuissima husababisha baka lenye umbo la ‘v’ kwenye sehemu za ncha za majani. Baadaye, kidonda cha rangi ya hudhurungi(kahawi iliyokolea) huenea hadi kwenye mshipa mkuu wa katikati na jani lote huwa na mwonekano uliojaa mabaka, hujikunja kuelekea ndani na kukakamaa (bakajani). Vidonda vinavyotokana na A. alternata ni vidogo, vina umbo la mviringo hadi umbo lisilo maalumu na huenea juu ya jani zima. Huanza kwa kubadilika rangi kuwa ya njano na vilivyotota maji, lakini vinapoongezeka, hugeuka kuwa sehemu yenye tishu/seli zilizo kufa na pia huathiri vishipajani vya karibu (doajani na kufa kwa tishu za mshipa). Sehemu za kati hukauka haraka na kumeguka, na kufanya jani kuwa na muonekano ulio toboka toboka/kuchanika na kusababisha mmea kupukutisha majani.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hakuna matibabu mbadala ya ufanisi ambayo yamepatikana dhidi ya ugonjwa huu hadi sasa. Kunyunyizia 3gramu/lita ya oksikloridi ya shaba baada ya kuonekana kwa dalili hufaa sana dhidi ya ugonjwa huu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Hatua za udhibiti wa kemikali ni pamoja na unyunyiziaji wa majani kwa mancozeb (3 gramu/lita ya maji) baada ya dalili za kwanza kuonekana.

Ni nini kilisababisha?

Magonjwa haya husababishwa na fangasi watatu wa aina ya Alternaria wanaoenezwa kwa njia ya udongo. Mbegu zilizoambukizwa zinaweza kuwa chanzo kikuu cha ugonjwa. Ikiwa zitapandwa wakati hali ya kimazingira ni rafiki, hasara kubwa inaweza kutokea. Maambukizi ya upili kati ya mmea mmoja na mwingine huwezeshwa na upepo na wadudu. Halijoto zaidi ya 20°C, majani kulowana kwa muda mrefu, na unyevu mwingi huchangia kuenea kwa ugonjwa huu. Matukio yanaweza kuwa mengi kwa mazao ya karanga yanayomwagiliwa wakati wa msimu wa baada ya mvua. Kulingana na kutokea na ukali wa ugonjwa, mavuno ya karanga na malisho yanaweza kupunguzwa hadi 22% na 63% mtawalia.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu kutoka kwenye mimea yenye afya au mbegu zilizothibitishwa ambazo hazina vimelea.
  • Tumia aina sugu au zinazostahimili.
  • Ondoa magugu, badilisha mimea inayohifadhi kuvu wa ugonjwa huu na mimea ya kujiotea yenyewe kutoka shambani.
  • Kagua shamba kwa ishara yoyote ya ugonjwa wakati wowote hali inapokuwa nzuri kwa vimelea vya magonjwa.
  • Ng`oa kwa mikono na uharibu mimea iliyoambukizwa inayopatikana kwenye vitalu vya mbegu au shambani.
  • Unashauriwa kufanya mzunguko wa mazao na mazao yasiyo hifadhi wadudu husika kwa angalau miaka mitatu.
  • Epuka kufanya kazi shambani wakati majani yamelowana.
  • Lima kwa kina ili kuondoa vimelea wowote waliobaki kwenye udongo.

Pakua Plantix