Mpunga

Doa-jani jembambala Kahawia la mpunga

Sphaerulina oryzina

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Vidonda vilivyo jipanga kwa mstari kwenye mhimili wa jani.
  • Kubadilika kwa rangi kwa vifuko-jani - "Doa la wavu".
  • Madoa ya baadaye huonekana.
  • Punje kuiva mapema kabla ya wakati.
  • Kubadilika kwa rangi ya hudhurungi ya mbegu au punje.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Mpunga

Dalili

Vidonda vya majani vilivyo katika mstari hukua hadi urefu wa 2-10 mm na kawaida sio zaidi ya 1-1.5 mm kwa upana. Mhimili wa ukuaji ni sambamba na ule wa jani. Vidonda vina kitovu cha hudhurungi-nyeusi na mpaka unaofifia kadiri ukingo wa nje unavyofikiwa. Vidonda kwenye kifuko-jani ni sawa na kwenye jani, wakati vidonda kwenye maganda ya mchele na vikonyo ni vifupi na huenea kwa ulalo. Katika aina sugu, vidonda vinaweza kuwa vyembamba, vifupi na vyeusi zaidi kuliko vilivyo kwenye aina zinazoshambuliwa kirahisi. Madoa huonekana katika hatua za baadaye za ukuaji, kabla ya kuanza kwa maua. Ugonjwa huu unaweza kusababisha punje kukomaa mapema na kubadilika kwa rangi ya hudhurungi ya mbegu au punje. Uangukaji wa mimea pia umeshuhudiwa.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hatujui matibabu yoyote mbadala dhidi ya Sphaerulina oryzina kwa sasa. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua kitu ambacho kinaweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ikiwa doa jembamba la kahawia litahatarisha shamba, nyunyiza propiconazole katika hatua tofauti za ukuaji wa mmea.

Ni nini kilisababisha?

Ugonjwa huu kwa kawaida hutokea kwenye udongo wenye upungufu wa potasiamu, na katika maeneo yenye joto kuanzia 25−28°C. Huonekana katika hatua za ukuaji wa baadaye wa zao la mpunga, kuanzia katika hatua ya kuchanua. Mimea ambayo ni wenyeji mbadala huruhusu kuvu kuishi na kuambukiza mazao ya mpunga kwa misimu mipya. Mimea huathirika zaidi wakati wa kuanza kwa masuke, na uharibifu unakuwa mbaya zaidi mimea inapokaribia kukomaa.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina sugu kama zinapatikana katika eneo lako.
  • Ondoa magugu na mimea ya kujiotea yenyewe shambani na maeneo jirani.
  • Panga uwekaji mbolea kwa usawa kwa msimu wote.
  • Hakikisha potasiamu ya kutosha inatumiwa.

Pakua Plantix