Monographella albescens
Kuvu
Dalili zinazohusiana na kubabuka kwa majani hutofautiana kulingana na hatua ya ukuaji, aina na msongamano wa mmea. Mara nyingi, vidonda vya kijani-kijivu, vilivyolowa maji huanza kutokea kwenye ncha au kingo za jani. Baadaye, vidonda huenea na kutoa muundo wa pete/mduara wa rangi ya kahawia-nyekundu na kahawia nyeusi kuanzia kwenye ncha za majani au kingo. Kuendelea kukua kwa vidonda husababisha kuungua kwa sehemu kubwa ya ubapa wa jani. Maeneo yaliyoathiriwa hukauka, na kufanya jani kuonekana kuungua. Katika baadhi ya nchi, vidonda mara chache huendeleza muundo wa pete/mviringo na ni dalili ya kuungua tu ndio inayoonekana.
Hakuna tiba mbadala iliyopatikana kufikia sasa dhidi ya ugonjwa huu.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matumizi ya thiophanate-methyl kwa matibabu ya kuloweka mbegu yalipunguza maambukizi ya M. albescens. Katika shamba, dawa za kunyunyuzia za majani zenye viua kuvu vya mancozeb, thiophanate methyl @1.0g/l au oksikloridi ya shaba hupunguza kwa kiasi kikubwa matukio na ukali wa kuungua kwa majani. Mchanganyiko wa kemikali hizi pia ni mzuri.
Ukuaji wa ugonjwa kwa kawaida hutokea mwishoni mwa msimu kwenye majani yaliyokomaa na hupendelewa na hali ya hewa ya mvua, urutubishaji mwingi wa naitrojeni, na nafasi ndogo kati ya mimea. Viwango vya naitrojeni zaidi ya kilo 40 kwa hekta na zaidi husababisha matukio ya kuungua kwa majani. Hukua kwa kasi katika majani yaliyo athirika kuliko katika majani yasiyoathirika. Vyanzo vya maambukizi ni mbegu na mabua ya mazao kutoka kwenye mavuno ya nyuma. Ili kutofautisha ugonjwa wa kuungua majani na baka-jani, zamisha majani yaliyokatwa kwenye maji safi kwa dakika 5−10; ikiwa hakuna utomvu unaotoka, basi ni ugonjwa wa kuungua majani.