Magnaporthe salvinii
Kuvu
Dalili kwa kawaida huonekana baada ya hatua ya mimea kuchipua mashina ya pembeni. Dalili za awali ni vidonda vidogo, vyeusi visivyo na mpangilio kwenye kifuko/ala ya nje ya jani karibu na usawa wa maji. Kadiri ugonjwa unavyoendelea, kidonda huongezeka, na kupenya ndani ya ala ya jani na shina na kutoa vidonda vya rangi ya kahawia-nyeusi. Pingili moja au mbili za shina hatimaye huoza na kuanguka (ngozi ya nje pekee ndiyo inayobakia bila kuharibiwa), na kusababisha mmea kuanguka, masuke yasiyojazwa, punje zenye unga kama chaki au kufa kwa mashina. Kuvu wa rangi ya kijivu iliyokolea wanaweza kuonekana ndani ya uwazi wa mashina yaliyoambukizwa, wenhye sclerotia ndogo nyeusi zilizo na alama juu ya uso wa ndani.
Mbinu za kudhibiti muoza wa shina ni pamoja na utaratibu mzuri wa usimamizi wa shamba, na matumizi ya viumbe kinzani.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Nyunyizia kemikali zenye validamycin au hexaconazole (2 ml/l), propiconazole (1 ml/l) au thiophanate methyl (1.0 g/l) mara mbili kwa muda wa siku 15, kwa kawaida kutoka hatua ya katikati ya kuchipua maote/mashina ya pembeni, au wakati wa ugonjwa kuanza.
Uharibifu husababishwa na fangasi Magnaporthe salvinii. Husalia msimu wote wa baridi ndani ya tishu za mmea uliokufa, au ndani ya udongo. Baadaye, wakati hali ni nzuri (unyevu mwingi, mbolea ya naitrojeni nyingi), vijimbegu vyake hutawanywa kupitia matone ya mvua na umwagiliaji wa maji. Vinapotua kwenye jani, hushikamana na uso wake na kutoa mrija wa vijidudu ambao huzama kupitia ngozi ya juu ya jani. Utaratibu huu unawezeshwa kwa mimea iliyo na majeraha kama matokeo ya matunzo mabaya au kushambuliwa na wadudu. Ukali wa magonjwa huongezeka wakati mazao yanakaribia kukomaa. Katika maeneo ya kitropiki, vipindi vya unyevu mwingi baada ya mavuno hupelekea mzunguko wa maisha wa kuvu.