Dengu Nyeusi & Kijani

Chule ya Choroko Nyeusi

Colletotrichum lindemuthianum

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa madogo yasiyo na mpangilio yenye unyevu kwenye majani, shina, vikonyo au maganda.
  • Madoa yaliyoungana huwa ni vidonda vilivyozama vyenye rangi ya weusi katikati na kingo angavu.
  • Vikwachu/vidonda kwenye mashina na vikonyo.
  • Kudondoka kwa majani.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Dengu Nyeusi & Kijani

Dalili

Maambukizi yanaweza kutokea katika hatua yoyote ya ukuaji wa mmea na huonekana kwenye majani, mashina, vikonyo, na maganda. Ikiwa maambukizi yatatokea baada ya mbegu kuota au ikiwa mbegu zimeathirika, miche itaonyesha madoa madogo ya kutu ambayo hukua taratibu na kuunda madoa makubwa ya umbo la jicho na hatimaye yanageuka na kuwa mabaka. Kwa mimea iliyokomaa, dalili za awali huonekana kama madoa madogo yasiyo na umbo maalumu yakiwa na maji maji na rangi ya kahawia iliyokolea hadi nyeusi, mara nyingi zaidi kwenye upande wa chini wa majani au vikonyo. Kadri muda unavyoenda, madoa haya hukua na kuwa vidonda vilivyozama vyenye sehemu za kati zenye giza na kingo za manjano, rangi ya machungwa au nyekundu angavu, na pia hutokea kwenye sehemu ya juu ya majani. Maganda huwa na vidonda vya rangi ya kutu na huweza kunyauka na kukauka. Katika hali ya maambukizi makubwa, sehemu za mmea zilizoathirika zinaweza kunyauka na kukauka. Kutokea kwa vikwachu (vidonda) kwenye mashina na vikonyo mara nyingi hufuatiwa na upukutikaji wa majani.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Vijidudu vya kibaiolojia (kama vile bakteria, virusi, na kuvu wa aina nyinge) vinaweza kusaidia kudhibiti maambukizi. Kuvu/ukungu aina ya Trichoderma harzianum na bakteria Pseudomonas fluorescens hutumika kama tiba za mbegu hushindana na kuvu anayesababisha ugonjwa huu. Dawa kuua kuvu za kupulizia ni pamoja na zile zinazotokana na copper oxychloride 3g/l kwa vipindi vya siku 15.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na tiba za kibaiolojia ikiwa zinapatikana. Matibabu ya ugonjwa kwa dawa za kikemikali huenda yasiwe na tija kiuchumi ikiwa hali ya hewa sio nzuri. Mbegu zinaweza kutiwa kwenye maji na kutibiwa kwa dawa sahihi za kuua kuvu/ukungu, kwa mfano thiram 80% WP @ 2 g/l au captan 75WP @ 2.5 g/l ya maji. Dawa za kuua ukungu za kupulizia ni pamoja na dawa zinazotokana na folpet, mancozeb, thiophanate methyl (0.1%) au copper oxychloride 3g/l zinazopaswa kupulizwa vipindi vya siku 15.

Ni nini kilisababisha?

Kuvu aina ya Colletotrichum lindemuthianum huishi kwenye udongo na kwenye mbegu na mabaki ya mimea yaliyoathirika. Pia huishi msimu wote wa baridi kwenye mimea mbadala inayohifadhi kuvu hawa. Vijimbegu(kwa jina lingine viiniyoga) vya kuvyu husafirishwa hadi kwenye miche inayokua kwa njia ya mvua, umande au kazi shambani wakati majani yakiwa na yamelowana. Hivyo ni muhimu kupunguza shughuli shambani (wafanyakazi, matibabu, n.k.) wakati majani yakiwa na maji maji kutokana na mvua au umande. Hali ya ubaridi hadi joto la wastani (13-21°C) na vipindi vya mvua za mara kwa mara, hayo ni mazingira muafaka kwa kuvu na usambaaji wake, hivyo kusababisha ongezeko lake na ukali/ukubwa wa maambukizi.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu zisizo na vimelea vya magonjwa zilizoidhinishwa.
  • Panda aina ya mbegu zinazostahimili au zenye ukinzani dhidi ya magonjwa.
  • Kagua mimea yako au mashamba ili kugundua uwepo wa ishara yoyote ya ugonjwa.
  • Epuka ukuaji wa magugu kupita kiasi (magugu yanaweza kuwa mwenyeji mbadala wa kuhifadhi vijidudu vya magonjwa) karibu na mazao yako.
  • Hakikisha shamba linakuwa safi.
  • Epuka kufanya kazi shambani wakati majani yakiwa na maji maji, na safisha zana na vifaa vyako vya kilimo.
  • Inashauriwa kufanya kilimo cha mzunguko wa mazao kwa kubadilisha na mazao yasiyohifadhi magonjwa kila baada ya miaka mitatu.
  • Baada ya mavuno, zika mabaki ya mimea iliyoathirika au yaondoe na yachome moto.

Pakua Plantix