Kabatiella zeae
Kuvu
Vidonda vidogo vidogo vilivyolotota maji na vya mviringo huonekana kwenye majani ya chini. Vidonda hivi hukua na kuwa "madoa jicho," kitovu cha rangi ya kahawia iliyokwajuka, kingo za kahawia iliyokolea, na duara kubwa lenye mwanga wa manjano. Baadaye huungana na kuunda mabaka ya manjano au tishu zilizokufa. Vidonda hivi hupatikana zaidi kwenye majani ya zamani, lakini vinaweza pia kuonekana kwenye vijalizo na maganda.
Samahani, hatujui matibabu yoyote mbadala dhidi ya ugonjwa wa DOA JICHO. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua jambo lolote linaloweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia kusikia kutoka kwako.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kukinga/kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Pima kwa umakini faida na hasara za kutumia dawa za kuua kuvu kwa kuangalia na uwezo wa kupatikana mavuno, thamani ya mazao, na gharama ya dawa za kuua kuvu. Matibabu kwa dawa za kuua kuvu ni pamoja na mancozeb, propiconazole, na chlorothalonil. Matibabu ya mbegu kwa kutumia dawa hizi pia yanaweza kuzingatiwa.
Kuvu huishi kwenye mabaki ya mahindi kwenye udongo na wanaweza pia kupatikana kwenye mbegu. Wakati wa majira ya kuchipua, huanza kuzalisha vijimbegu ambavyo huenezwa kwenye mazao mapya kwa njia ya upepo au matone ya mvua. Uenezwaji wa upili unatokea kupitia upepo na matone ya maji ya viinimbegu kutoka mmea mmoja hadi mwingine. Majimaji kwenye majani, halijoto ya ubaridi, mvua za mara kwa mara au umande huchochea mlipuko wa ugonjwa. Hali ya joto na ukavu, kwa upande mwingine, husaidia kupunguza maendeleo yake. Ulimaji wa zao moja tu shambani na mbinu za kupunguza namna ya ulimaji wa kawaida pia kunanufaisha maendeleo ya kuvu. Ikiwa kuvu inaenea hadi sehemu za juu za mmea wakati wa hatua za kutoa maua au kukomaa kwa mahindi, inaweza kupunguza tija ya mmea na mavuno.