Fusarium virguliforme
Kuvu
Madoa madogo ya kijani hafifu ya mviringo yanaonekana kwenye majani wakati wa kipindi cha maua. Mabadiliko ya rangi ya manjano kati ya vishipa-jani na baadaye tishu zilizo kufa huonekana kwenye majani. Kadiri ugonjwa unavyo endelea, tishu za zilizo kufa katikati ya mishipa zinaweza kufa na kudondoka, na kufanya majani kuwa na mwonekano wa kuchanika. Majani hatimaye yanaweza kukauka, kujikunja au kudondoka lakini vikonyo vinabaki kushikamana na shina. Dalili za kuoza (kubadilika rangi ya kahawia) huonekana kwenye tishu za ndani za sehemu ya chini ya shina na mzizi mkuu. Maua yanaweza kudondoka mapema na maganda yanaweza yasikue au kujaa punje.
Hadi leo, hakuna udhibiti wa kibiolojia wa kuvu huyu unaojulikana. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unafahamu yoyote.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuvu za kunyunyizia majani hazifanyi kazi kwa sababu kuvu hubaki kwenye mfumo wa mizizi. Badala yake, weka dawa maalumu za kuua kuvu, kama vile fluopyram kwenye mbegu.
Kuvu Fusarium virguliforme hudumu kama vijimbegu kwenye udongo au kwenye mabaki ya mazao yaliyoshambuliwa. anaambukiza na kutawala mimea kupitia mizizi mapema katika hatua ya ukuaji, lakini dalili zinaweza kuonekana tu wakati wa maua. Maambukizi hupendelea udongo ulio poa na ulio lowana, hali ya hewa ya mvua, mashamba yaliyopandwa kwa msongamano mkubwa, mifumo duni ya kupitisha maji au udongo ulioshikana. Majeraha ya minyoo ya uvimbe wa soya, wadudu na majeraha ya mitambo kutokana na ushughulikiaji mbaya pia hupelekea hatari ya kuambukizwa.