Cercospora kikuchii
Kuvu
Dalili za wazi huonekana katika hatua za ukuaji wa baadaye, wakati kuweka maua na matunda. Ugonjwa huu una sifa ya kuwepo kwa madoa yanayo badilika rangi kutoka rangi ya zambarau hadi kahawia kwenye sehemu ya juu ya majani na muonekano wa kuungua na jua. Madoa mekundu-kahawia yanaweza pia kuonekana kwenye mashina na maganda ya mbegu. Mbegu zilizoambukizwa zinaweza kuonekana zenye afya au kuwa na mabadiliko ya rangi toka pinki hadi zambarau yenye ukubwa tofauti kutoka madoa madogo hadi mabaka makubwa kwenye ganda la mbegu. Hii inaweza isiwe na athari mbaya kwenye mavuno, lakini viwango vya mbegu kuota na kukua kwa miche vinaweza kuathiriwa.
Samahani, hatujui matibabu yoyote mbadala dhidi ya vimelea hivi vya kuvu (Cercospora kikuchii) . Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua kitu ambacho kinaweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia kusikia kutoka kwako.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Kwenye eneo lenye asilimia kubwa ya mbegu zilizobadilika rangi tibu mbegu kwa dawa za kuua kuvu. Hii inaweza kutoa udhibiti fulani juu ya kuenea kwa ugonjwa huo. Zingatia kutumia dawa za kuua kuvu/ukungu kwenye majani, kwa mfano mancozeb (2.5 g/lita ya maji) katika hatua za awali za mmea kuzaa ili kuzuia ukungu kwenye majani na maambukizi ya maganda ya mbegu.
Doa Zambarau la Mbegu ya Soya husababishwa na Cercospora kukuchii. Kuvu hawa huishi msimu mzima wa majira ya baridi kwenye mabaki ya mimea chini ya udongo na kwenye mbegu. Unyevu mwingi, halijoto ya wastani (kuanzi 22 hadi 26°C), upepo na matone ya mvua hupelekea kuenea kwa Kuvu kwenye majani na kukua kwa ugonjwa. Maambukizi ya awali mara nyingi huwa yamefichika na hayaonekani hadi wakati wa maua au uundaji wa matunda/maganda ya soya. Kuvu huingia kwenye ganda polepole na kukua kwenye mbegu, na kuzipa madoa ya rangi ya zambarau au kahawia.