Rhizoctonia solani
Kuvu
Mwanzoni, madoa ya kijani ya mviringo au yasiyo na umbo maalumu yaliyotota maji yenye kingo za rangi ya kahawia-nyekundu huonekana kwenye majani ya zamani, wakati mwingine kwenye vipande vya majani tofauti. Katika hatua za baadaye za ugonjwa huo, vidonda hugeuka kuwa na rangi ya kahawia au hudhurungi, na madoa huanza kuonekana kwenye vikonyo, shina na maganda machanga. Mibenuko/mikunjo ya kahawia hukua kwenye shina na vikonyo. Miunganiko ya majani na ukuaji wa kuvu kama pamba pia ni kawaida. Maambukizi makali husababisha mnyauko wa majani na maganda na kupukutika kwa majani. Maambukizi ni ya kawaida zaidi katika hatua za mwishoni za ukuaji wa mimea.
Mawakala wa kibaiolojia, viziduo/vimiminika vya mimea na mafuta ya mimea vinaweza kusaidia kudhibiti maambukizi. Kuvu wa vimelea aina ya Trichoderma harzianum hushindana na Baka-Rhizoctonia la Sehemu za Juu za Mmea. Viziduo vya mimea ya vitunguu, vitunguu saumu na bizari hupunguza ukuaji wa kuvu, kwa utaratibu huu wa ufanisi. Mafuta ya mimea ya mentha, citronella, peppermint, palmarosa na geranium yanaweza kuzuia maambukizi kuongezeka.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Ikiwa dawa za kuua kuvu zinahitajika, nyunyiza bidhaa zenye fluxapyroxad pamoja na pyraclostrobin. Tumia dawa za kuua kuvu si zaidi ya mara mbili kwa msimu. Usianze matibabu ikiwa kuna chini ya siku 21 za kuvuna.
Kuvu Rhizoctonia solani huishi kwenye udongo au kwenye uchafu wa mimea. Anaweza kusalia kwa msimu wote wa baridi katika mimea mbadala kama vile magugu. Wakati wa vipindi virefu vya joto (25 hadi 32 ° C) na unyevu mwingi, fangasi huenea sana kwenye mimea kutokana na upepo na mvua. Wanasuka majani pamoja na kutengeneza mikeka ya majani "ya utando", na kuupa mmea sifa hiyo.