Mahindi

Muozo Fusari wa Gunzi

Fusarium verticillioides

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Mbegu zinakuwa na ukungu (kuvu) mweupe, wenye rangi ya waridi (pinki).
  • Uwepo wa michirizi yenye rangi ya hudhurungi inayofuata muundo wa duara.
  • Gunzi lililonyauka na punje zilizooza.
  • Kutokana na hali hiyo, punje zinakuwa haziwezi kuliwa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Mahindi

Dalili

Dalili zinatofautiana kutegemea na aina ya mahindi, mazingira na ukubwa wa ugonjwa. Ugonjwa huu kwa kawaida hujitokeza mwishoni mwa msimu na wakati wa kuhifadhi mahindi. Nafaka zenye ugonjwa zikiwa na ukungu mweupe, na rangi ya waridi (pinki) husambaa katikati ya zile zinazoonekana kuwa na afya. Nafaka hizo zinaweza pia kuonyesha mabadiliko ya rangi. Zinaweza kubadilika na kuwa na rangi ya hudhuringi au kahawia. Mabadiliko haya ya rangi yanafuata muundo wa mduara kutokea juu ya nafaka. Ikiwa hali iliyopo ni muafaka kuchochea kutokea kwa ugonjwa (yaani kuna hali ya hewa ya joto la kiasi na ukavu, uwepo wa wadudu), masuke yanaweza kukaliwa kabisa na kuvu na kuonyesha ukuaji mkubwa wa kuvu. Suke zima huonekana kama limenyauka na nafaka zinaweza kuteketezwa kabisa. Mavuno ya nafaka yanapungua. Kuvu (ukungu) huzalisha sumu, na hivyo kufanya masuke yasiwe salama kwa kula.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Mchanganyiko unaotokana na bakteria aina ya Pseudomonas fluorescens unaweza kutumika kama matibabu ya mbegu na kwa kupulizia ili kupunguza uwepo wa ugonjwa na uzalishaji wa sumu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Utumiaji wa dawa za kuua kuvu mwanzoni mwa msimu inaweza kupunguza maambukizi ya masuke. Kwa kuwa uharibifu unatokea kwenye masuke, dawa za kuua kuvu sio njia yenye ufanisi zaidi katika kupambana na ugonjwa. Fikiria kudhibiti wadudu waharibifu wanaojeruhi masuke na kuchochea ukuaji wa kuvu. Dawa zenye propiconazole 1 ml/l zinaweza kutumika katika hatua punje zinapokuwa ngumu ili kudhibiti kuvu.

Ni nini kilisababisha?

Ugonjwa huu unasababishwa kuvu ambae kitaalamu anafahamika kama Fusarium verticillioides, lakini aina nyingine za Fusari zinaweza kusababisha dalili sawa na za ugonjwa huu. Kuvu hawa huishi kwenye mbegu, mabaki ya mazao au kwenye mimea mwenyeji ambayo kuvu hawa wanaweza kuishi kwa muda; na mimea hiyo ni kama vile majani. Vijimbegu (viiniyoga) vya kuvu husambazwa hasa kwa njia ya upepo. Vijimbegu hivi hupenya kwenye masuke ya mahindi hasa kupitia majeraha yanayosababishwa na mvua za mawe au uharibifu unaotokana na wadudu na ndege kula sehemu za mmea, au majeraha yanayosababishwa na kazi za shamba. Vijimbegu vya kuvu huota na taratibu hujaa kwenye punje za mahindi kuanzia sehemu ya kuingiliaa. Vinginevyo, vinaweza kuanza kujaa kwenye mmea kuanzia kwenye mizizi na kupanda juu ya mmea kupitia ukuaji wa mfumo mzima. Mimea inaweza kuambukizwa katika hali ya mazingira mbalimbali, lakini dalili huwa mbaya zaidi wakati hali ya hewa ni ya joto la wastani na yenye ukavu na mimea ikiwa imefikia hatua ya kutoa maua. Hii ni aina ya ukungu inayopatikana zaidi kwenye mahindi.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina za mbegu zinazostahimili au kuvumilia magonjwa zinazopatikana sokoni.
  • Panda mimea inayoendana na hali ya hewa ya eneo lako.
  • Epuka kupanda mimea kwa msongamano.
  • Hakikisha kunakuwa na uwekaji sahihi wa mbolea katika hatua za baadaye za ukuaji wa mimea.
  • Safisha nafaka zilizoathirika na ugonjwa au zihifadhi peke yake ili kuepusha utengenezwaji wa sumu.
  • Safisha vizuri sehemu ya kuhifadhia nafaka.
  • Fuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa kabla ya kuvuna mazao ili kuepuka kulowana kwa mazao katika sakafu ya kupukuchua mahindi.
  • Hakikisha huumizi mazao wakati wa kuvuna.
  • Hifadhi nafaka katika unyevu anga wa chini na joto la chini.
  • Katua na yazike mabaki ya mazao baada ya kuvuna.
  • Fanya mzunguko wa mazao kwa kubadilisha na mazo yasiyoambukizwa au kuhifadhi vimelea vya ugonjwa huu kwa angalau mwaka mmoja.

Pakua Plantix