Mpunga

Muozo wa Kifuko-jani cha Mpunga

Sarocladium oryzae

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Vidonda kama doa kwenye ala/vifuko-jani vya majani ya juu.
  • Kuoza kwa ala/vifuko-jani.
  • Ukuaji wa ukungu mweupe na wa unga na nafaka zilizobadilika rangi.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Mpunga

Dalili

Dalili za awali ni madoa ya mstatili hadi madoa yasiyo na umbo maalumu kwenye majani (0.5 hadi 1.5 mm) ambayo huzunguka suke. Madoa yana sifa ya vitovu vya kijivu na ukingo wa kahawia na mara nyingi huunganishwa na kuunda muozo na kisha kubadilika kwa rangi ya ala za majani. Katika maambukizi makubwa, masuke machanga hayawezi kujitokeza. Ala za majani zilizoathiriwa zinaweza kuwa na unga mwingi mweupe wa kuvu unaoonekana kwenye uso wa nje. Nafaka za masuke yaliyoibuka hubadilika rangi na kuwa tasa. Masuke ambayo hayajajitokeza hutoa maua ambayo hubadilika kuwa mekundu-kahawia hadi hudhurungi iliyokolea. Maambukizi hudhuru zaidi yanapotokea katika hatua za baadaye za kuchanua na yanaweza kusababisha uharibifu mkubwa.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Bakteria kama vile Rhizobacteria wa Pseudomonas fluorescens waliotengwa kutoka kwenye machungwa na mpunga ni sumu kwa kuvu wa muozo wa ala ya jani la mpungu, na kusababisha matukio machache na mavuno mengi. Bipolaris zeicola ni mpinzani mwingine anayewezekana wa muoza wa ala ambae anaweza kuzuia kabisa ukuaji wa mycelial wa S. oryzae. Shughuli ya kudhibiti kuvu ya viziduo kutoka kwenye majani na maua ya Tagetes erecta pia huzuia S. oryzae mycelium kwa 100%.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Iwapo mashambulizi ni makali, utumiaji wa dawa za kuua kuvu kama vile mancozeb, oxychloride ya shaba au propiconazole (kawaida 1 ml/l ya maji) wakati wa kupanda na kuibuka kwa masuke kila baada ya wiki kunaweza kupunguza matukio ya ugonjwa huo. Utumiaji wa dawa ya kutibu mbegu kama vile mancozeb kabla ya kupanda pia ni mzuri.

Ni nini kilisababisha?

Kuoza kwa ala ni ugonjwa unaoenezwa na mbegu. Ugonjwa huu husababishwa hasa na fangasi Sarocladium oryzae lakini pia katika baadhi ya matukio na Sacroladium attenuatum. Kuvu huishi kwenye mabaki ya zao la mpunga baada ya kuvuna na wanaweza kusababisha maambukizi katika misimu inayofuata. Matukio yake huongezeka kwa kuongezeka kwa msongamano wa upandaji na katika mimea ambayo hutoa sehemu za kuingilia kwa kuvu, kwa namna ya majeraha na vidonda vinavyosababishwa na wadudu katika hatua ya kuanza kwa masuke. Uwekaji wa potasiamu, sulfeti ya kalsiamu au mbolea ya zinki katika hatua ya kuchipua mashina ya pembeni huimarisha tishu za shina na majani na hivyo kuepuka uharibifu mkubwa. Pia huambatana na mimea iliyo dhoofishwa na maambukizi ya virusi. Hali ya hewa ya joto (20-28°C) na yenye unyevunyevu (mvua) huchangia ukuaji wa ugonjwa.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu zenye afya, ikiwezekana kutoka kwa vyanzo vilivyoidhinishwa.
  • Tumia umbali mpana wa kupanda wa 25cm x 25cm.
  • Epuka kilimo cha zao moja katika shamba moja kwa kutumia angalau aina mbili.
  • Chunguza mashamba mara kwa mara ili kuona wadudu waharibifu kama vile utitiri wa suke na jaribu kuwadhibiti.
  • Weka mbolea ya potasiamu, salfeti ya kalsiamu au zinki katika hatua ya kuchipua mshina ya pembeni.
  • Uondoaji wa mabua na magugu yaliyo ambukizwa shambani pia husaidia.

Pakua Plantix