Cochliobolus heterostrophus
Kuvu
Dalili zitatofautiana kidogo kutegemea na nguvu ya vimelea, aina ya mmea, na hali za mazingira. Vidonda vyenye rangi ya hudhurungi vikianza kwa kuwa na umbo la almasi na hatimae kurefuka huku vikiwa na kingo za kahawia hutokea kwanza kwenye majani ya chini na kisha polepole vinasonga juu hadi kwenye majani machanga. Mabaka hayo huwa na ukubwa tofauti na huenea hadi kuvuka mishipa ya majani. Katika mimea iliyo kwenye hatari ya kuathirika, vidonda vinaweza kuungana, na kusababisha mabaka yanayofunika kabisa sehemu kubwa za majani. Magunzi ya mahindi pia yanaweza kuonyesha kufunikwa na vitu vya kijivu na kuharibika kwa umbo katika hatua za baadaye za ugonjwa. Upoteaji wa tija kutokana na uharibifu wa majani unaweza kusababisha mimea kukauka na kuvunjika mashina yake. Mimea inaweza kuanguka.
Udhibiti wa kibaiolojia kwa kutumia kuvu mshindani aitwae Trichoderma atroviride SG3403 umetumika kwa mafanikio dhidi ya maambukizi ya vimelea. Hata hivyo, majaribio ya shambani bado yanahitajika ili kuthibitisha ufanisi wa matibabu haya kwenye mashamba.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga pamoja na hatua za udhibiti wa kibaiolojia ikiwa zinapatikana. Matumizi ya dawa za kuua kuvu/ukungu yanaweza kudhibiti ugonjwa kwa ufanisi ikiwa zitatumiwa kwa wakati sahihi. Fikiria kutumia dawa za kuua kuvu baada tu ya kutathmini maendeleo ya ugonjwa dhidi ya upotevu wa mavuno unaoweza kutokea, utabiri wa hali ya hewa, na hatua ya ukuaji wa mimea. Inapendekezwa kutumia aina yoyote ya dawa zinazofanya kazi kwa haraka na zinazoweza kuua aina nyingi ya vimelea wa kuvu, na dawa hizi ni kama vile mancozeb (2.5 g/l) ikitumika kila baada ya siku 8-10.
Ugonjwa unasababishwa na kuvu aitwae Cochliobolus heterostrophus (pia hufahamika kama Bipolaris maydis). Kuvu hawa huishi kwenye mabaki ya mimea yaliyoko kwenye udongo. Wakati hali ni nzuri, kuvu huzalisha vijimbegu/viiniyoga ambavyo huenezwa kwenye mimea mipya kwa upepo na matone ya mvua. Vijimbegu huota kwenye majani na kukamilisha mzunguko wake kamili wa maisha (kutoka maambukizi hadi uzalishaji mpya wa vijimbegu vya kuvu) ndani ya saa 72. Ukuaji wa kuvu na mchakato wa maambukizi unafanikishwa na hali ya hewa yenye unyevunyevu, maji maji kwenye majani, na joto la kati ya 22 hadi 30°C. Uharibifu kwenye majani hupunguza tija (uzalishaji) ya mmea na unaweza kupunguza mavuno ikiwa maambukizi yanatokea mwanzoni mwa msimu.