Mahindi

Doa Jani la Phaeosphaeria

Phaeosphaeria maydis

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa madogo, yenye rangi ya kijani hafifu hadi manjano yaliyotawanyika kwenye ubapa wa jani.
  • Madoa haya hukua na kuwa vidonda vyenye umbo la mviringo au mstatili, vyenye sehemu za katikati zilizokauka na kufifia, huku yakiwa na kingo zisizo za kawaida zenye rangi ya kahawia iliyokolea.
  • Katika hali mbaya, madoa haya huungana na kusababisha mabaka kwa jani zima.
  • Ugonjwa wa Baka Jani wa Phaeosphaeria kwa kawaida huchukuliwa kama ugonjwa wa mwishoni mwa msimu ulio na umuhimu mdogo.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Mahindi

Dalili

Dalili za awali huonekana kama madoa madogo, yenye rangi ya kijani hafifu hadi manjano yaliyotawanyika kwenye ubapa wa jani. Baadaye, madoa haya huongezeka ukubwa na kuwa vidonda vyenye umbo la mviringo au mstatili (3 to 20 mm), vyenye sehemu za katikati zilizopauka na kukauka, na kingo zisizo za kawaida zenye rangi ya kahawia iliyokolea. Katika hali mbaya, madoa haya huungana na kusababisha mabaka kwa jani zima. Vijidoa vidogo vyeusi huonekana ndani ya vidonda kwenye upande wa chini wa majani. Ikiwa maambukizi yanatokea katika hatua za mwanzo za ukuaji wa mmea na majani ya juu yanakuwa na mabaka kabla ya mmea kutoa maua, inaweza kusababisha upotevu mkubwa wa mavuno.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Samahani, hadi sasa hatufahamu uwepo wa tiba yoyote ya kibaolojia kwa ugonjwa huu. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unafahamu chochote kinachoweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia kusikia kutoka kwako.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye kutumia hatua za kinga pamoja na hatua za kudhibiti kibaolojia ikiwa zinapatikana. Dawa za kuua kuvu kama vile mancozeb na pyraclostrobin zinaweza kupuliziwa kwenye majani ili kudhibiti ugonjwa huu.

Ni nini kilisababisha?

Ugonjwa huu unasababishwa na kuvu/fangasi anayefahamika kama Phaeosphaeria maydis, ambae huishi kwenye mabaki ya mazao wakati wa majira ya baridi. Katika hali za hewa zinazofaa, vijimbegu (viininyoga) vyake huenezwa kwenye mimea mipya kupitia rasharasha za mvua na upepo. Vijimbegu (viiniyoga) humea kwenye majani mapya na kuanzisha hatua ya pili ya maambukizi. Mvua nyingi na unyevunyevu wa juu kiasi (zaidi ya 70%) pamoja na joto kiasi la usiku (takriban 15°C), huchochea maendeleo ya ugonjwa huu. Hali hizi hupatikana zaidi katika maeneo ya ukanda wa juu. Ugonjwa huathiri tija ya mazao na mavuno katika hali maalum tu. Kwa ujumla ugonjwa huu huchukuliwa kama ugonjwa wa mwishoni mwa msimu ulio na umuhimu mdogo.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina ya mimea inayostahimili ugonjwa ikiwa inapatikana katika eneo lako.
  • Panda mapema au kwa kuchelewa ili kuepuka hali ya hewa inayochochea kuenea kwa ugonjwa huu.
  • Lima kwa kwenda chini zaidi (kina) na yazike mabaki ya mazao baada ya kuvuna.

Pakua Plantix