Papai

Ugonjwa wa Baka Jeusi la Papai

Asperisporium caricae

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa ya kahawia kwenye majani ya chini.
  • Madoa hutanuka, hutengeneza upele mweusi wenye unga unga.
  • Vidonda vya juu juu, vya rangi ya kahawia nyepesi na rangi nyeusi katikati, kwenye matunda.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Papai

Dalili

Mwanzoni, madoa yenye utomvu yaliyotawanyika, wakati mwingine huwa na halo ya njano, huonekana kwenye majani ya chini. Kwenye upande wa chini wa majani, madoa haya baadaye hutanuka na kuwa upele mweusi wenye unga wenye kipenyo cha hadi 4 mm. Katika hatua za baadaye za ugonjwa huo, seli katika vidonda hivyo hufa na vinaweza kuchukua sehemu kubwa za jani. Katika maambukizi makali au maambukizo ya pamoja na vimelea vingine vya kuvu, majani yenye ugonjwa yanaweza kudondoka, na kusababisha kuzuia ukuaji katika miti iliyoathiriwa. Vidonda visivyo na kina, vyenye rangi ya kahawia nyepesi, visivyo na mpangilio na matundu meusi ya kuvu kwenye sehemu ya katikati pia huonekana kwenye matunda yenye ugonjwa, ingawa kwa kiasi kidogo kuliko kwenye majani. Kudondoka mapema kunaweza kutokea endapo matunda yatambukizwa katika hatua za mwanzo za ukuaji. Licha ya vidonda, nyama ya matunda haionyeshi dalili za kuoza.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hakuna matibabu mbadala dhidi ya Asperisporium cariccae ambayo yamegunduliwa hadi sasa. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua kitu ambacho kinaweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia kusikia kutoka kwako.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Kunyunyizia dawa za kuua kuvu kama vile dithiocarbamates kunaweza kuwa na ufanisi endapo maambukizi/mashambulizi ni makali/makubwa.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na kuvu/fangasi aina ya Asperisporium caricae. Wanapatikana hasa Amerika ya Kati na sehemu za magharibi za Amerika Kusini na Afrika Mashariki. Majani na matunda yote yanaweza kuathiriwa na dalili hutofautiana kidogo kulingana na aina ya mazao na hali ya mazingira. Ugonjwa huo ni mkali zaidi kwenye majani ya chini, na wakati wa hali ya hewa yenye unyevunyevu. Papai ndio mwenyeji pekee wa vimelea hivi na kwa kawaida huwa na athari ndogo kwa sababu dalili za kwenye matunda kwa kawaida hubakia juu juu. Hata hivyo, ugonjwa huo unaweza kusababisha kupungua kwa ubora wa matunda.


Hatua za Kuzuia

  • Ondoa na uharibu sehemu za mmea zenye ugonjwa au matunda yaliyoanguka.

Pakua Plantix