Colletotrichum sp.
Kuvu
Vidonda vya mduara au vyenye pembe vilivyotota maji kwenye matunda ambavyo baadaye huwa laini na vilivyozama kidogo. Sehemu za katikati ya vidonda zina rangi ya chungwa au kahawia na hubadilika kuwa nyeusi wakati tishu zilizo karibu zina rangi nyepesi. Vidonda vinaweza kufunika sehemu nyingi za matunda. Vidonda vingi hutokea. Miduara yenye kitovu shiriki ni kawaida ndani ya madoa ya matunda. Matunda ya kijani yanaweza kuambukizwa lakini hayaonyeshi dalili zozote hadi yatakapo iva. Dalili za majani na shina huonekana kama madoa madogo yasiyo na umbo maalumu yenye rangi ya kijivu-kahawia na ncha za kahawia iliyokolea. Mwishoni mwa msimu, matunda yaliyoiva huoza na kufa kwa matawi kutokea juu kuelekea chini.
Mbegu zilizo ambukizwa zinaweza kutibiwa kwa kulowekwa kwenye maji moto ya 52°C kwa dakika 30. Joto na muda vinapaswa kuzingatiwa kwa usahihi ili kupata matokeo ya matibabu yanayotakiwa.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ikiwa dawa za kuua ukungu zinahitajika, nyunyiza bidhaa zenye mancozeb au bidhaa zinazo tokana na shaba. Anza matibabu wakati mimea inaweka maua.
Ugonjwa huu husababishwa na kundi la fangasi wa jenasi ya Colletotrichum, miongoni mwao ni C. gloeosporioides na C. capsici. Viini hivi vya magonjwa vinaweza kuambukiza mimea ya pilipili katika hatua zote za ukuaji, kwenye matunda machanga na vile vile kwenye matunda yaliyokomaa, na baada ya kuvuna. Wanaishi ndani na nje ya mbegu, kwenye uchafu wa mimea au kwenye mimea mingine jamii ya Solanaceae. Wanaweza pia kuletwa upya kupitia vipandikizaji vilivyoambukizwa. Kuvu hustawi wakati wa joto na mvua, na wanaweza kuenea kupitia mvua au maji ya umwagiliaji. Maambukizi ya matunda yanaweza kutokea kwenye joto kuanzia 10 ° C hadi 30 ° C, wakati 23 ° C hadi 27 ° C ni joto linalofaa zaidi kwa maendeleo ya ugonjwa. Maji maji kwenye uso wa matunda huongeza ukali wa chule.