Muwa

Kutu ya Kawaida ya Miwa

Puccinia melanocephala

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Dalili za awali ni madoa marefu ya majani yenye rangi ya manjano.
  • Madoa hubadilisha rangi polepole hadi nyekundu-kahawia.
  • Majani yaliyoathiriwa sana yanaweza kuwa na tishu zilizokufa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Muwa

Dalili

Dalili za awali za kutu ya kawaida ya miwa ni madoa marefu ya majani yenye rangi ya manjano, yenye urefu wa 1-4 mm. Pamoja na maendeleo ya ugonjwa (haswa kwenye uso wa chini wa jani) madoa hurefuka sambamba na mishipa ya jani. Yanapanuka hadi 20 mm kwa urefu na mm moja hadi tatu kwa upana. Pia hubadilika kuwa na rangi ya machungwa-kahawia au nyekundu-kahawia na mduara angavu mdogo wa manjano lakini dhahiri. Baadaye, upele wa kutu huungana. Hii inasababisha kupasuka kwa ngozi ya juu ya majani na kukua kwa maeneo yenye tishu zilizokufa. Vidonda kawaida huwa nyingi karibu na ncha ya jani na hupungua kwa idadi kuelekea kitako cha jani.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Samahani, hatujui matibabu yoyote mbadala dhidi ya Puccinia melanocephala . Tafadhali wasiliana nasi ikiwa unajua kitu ambacho kinaweza kusaidia kupambana na ugonjwa huu. Tunatarajia kusikia kutoka kwako.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu kwa dawa za kuua kuvu yanaweza kuwa mabaya kiuchumi na hayafai.

Ni nini kilisababisha?

98% ya unyevunyevu na usiku wa baridi ikifuatwa na siku zenye joto na halijoto kati ya 20°C na 25°C hupelekea kutu ya kawaida. Mwendelezo wa nyevu wa majani ( kwa saa tisa au zaidi) pia husaidia kuenea kwa ugonjwa huu. Chini ya hali nzuri mzunguko wa maambukizi ya kutu ya kawaida (Puccinia melanocephala) ni chini ya siku 14 kwa muda mrefu. Mimea yenye umri wa miezi miwili na sita huathirika zaidi na kutu ya kawaida.


Hatua za Kuzuia

  • Kuza aina sugu.
  • Hakikisha usawa wa lishe ya udongo.
  • Hakikisha ugavi wa maji wa kutosha kwenye udongo wakati wa ukuaji.
  • Weka mifereji mirefu au njia za upandaji wa mistari iliyooanishwa.
  • Ondoa na choma mabaki na ukusanye takataka za mazao yaliyoathirika.

Pakua Plantix