Mzeituni

Bakajani la Mzeituni

Venturia oleagina

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa meusi, yenye masizi kwenye uso wa juu wa majani, hukua hatua kwa hatua.
  • Duara lenye mwanga wa manjano (halo) kuzunguka kila doa.
  • Kudondoka kwa majani, matawi kufa, na kushindwa kutoa maua kunaweza kutokea.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Mzeituni

Mzeituni

Dalili

Mwishoni mwa majira ya kuchipua, madoa yenye masizi (yajulikanayo kama madoa ya tausi) huonekana kwenye sehemu ya juu ya majani yaliyoko katika matawi ya chini kwenye mimea. Madoa haya yanaweza pia kuonekana kwenye shina na matunda, lakini hupatikana zaidi kwenye uso wa jani. Upande wa chini wa majani hauonyeshi dalili zozote dhahiri. Msimu unapoendelea, madoa meusi hukua na yanaweza kufunika sehemu kubwa ya jani (kipenyo cha sm 0.25 hadi 1.27). Halo ya manjano polepole huibuka kazunguka madoa haya na kuenea kwenye jani zima. Miti inaweza kupukutisha/kudondosha majani na katika hali mbaya zaidi matawi hukauka/kufa. Maua yanaweza pia kushindwa kutokea, na kusababisha kupungua sana kwa uzalishaji wa mazao.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Nyunyiza majani ya miti kwa misombo (michanganyiko) ya kikaboni ya shaba kama vile mchanganyiko wa Bordeaux baada ya matunda kuvunwa katika msimu wa vuli na tena mwishoni mwa msimu wa baridi ikiwa kuna mvua za masika za mara kwa mara.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia endapo yanapatikana. Nyunyiza majani ya miti kwa misombo ya shaba (copper hydroxide, copper oxychloride, tribasic copper sulfate, na copper oxide ) baada ya matunda kuvunwa katika msimu wa joto na tena mwishoni mwa msimu wa baridi ikiwa mazingira yana mvua nyingi.

Ni nini kilisababisha?

Dalili hizo husababishwa na kuvu aitwae Fusicladium oleagineum, ambae hustawi katika maeneo ya nyanda za chini au katika mazingira ambayo hupokea mwanga kidogo wa jua au yenye kivuli kikubwa cha miti iliyokutana kwa juu. Kuvu huyo huhitaji joto la wastani hadi la chini na unyevu wa kutosha kwenye majani ili kuchipua na hivyo husababisha maambukizi wakati wa mvua katika vuli, msimu wa baridi na masika. Ukungu, umande na unyevu mwingi ni mambo muhimu yanayochangia kuenea kwa ugonjwa huo. Kinyume chake, hali ya joto na kavu katika majira ya kiangazi husababisha kuvu kuto kuendelea kuzaliana na hatimaye ukuaji wake husimama kabisa. Hii huonyeshwa na mabadiliko ya rangi ya madoa, ambayo hugeuka kuwa meupe na yenye gamba. Majani machanga huathirika zaidi na maambukizi kuliko yaliyokomaa/kuzeeka. Kiwango cha joto kinachopendelewa ni 14-24 °C, hata hivyo anaweza kustahimili pia kiwango kati ya 2-27 °C. Upungufu wa virutubisho au uwiano usio sahihi katika udongo unaweza pia kuongeza uwezekano wa miti ya mizeituni kushambuliwa. Kwa mfano, kuzidi kwa naitrojeni na upungufu wa kalsiamu hufikiriwa kudhoofisha kinga ya miti ya mizeituni dhidi ya magonjwa.


Hatua za Kuzuia

  • Fuatilia/kagua shamba mara kwa mara kujua dalili za ugonjwa huu.
  • Epuka kutumia mbolea zenye kiasi kikubwa cha naitrojeni na upungufu wa kalsiamu.
  • Chagua aina sugu au zinazo stahimili, ikiwa zinapatikana katika eneo lako.

Pakua Plantix