Mlozi

Baka Jani Jekundu la Mlozi

Polystigma ochraceum

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa ya kijani iliyopauka hadi rangi ya chungwa au madoa meusi yaliyokaa bila mpangilio kwenye majani huku yakiwa yamezungukwa na duara lenye mwanga la rangi ya kahawia.
  • Majani ya kujikunja na kukauka kutoka kwenye ncha au kingo.
  • Udondokaji majani mapema unaweza kutokea.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Mlozi

Mlozi

Dalili

Dalili huanza kama madoa ya kijani iliyopauka kwenye pande zote za majani, na baadaye kugeuka kuwa mabaka ya rangi ya manjano-machungwa. Madoa haya hukua kwa ukubwa katika kipindi chote cha majira ya kuchipua na hatua kwa hatua huanza kuungana na kufunika sehemu kubwa ya lamina mwishoni mwa majira ya joto. Kadri madoa yanavyoenea, katikati yake kunakuwa na weusi usio na mpangilio, ukizungukwa na duara la mwanga lenye rangi ya kahawia. Katika hatua za juu za ukuaji wa ugonjwa, majani hujikunja na hatimae tishu zake hufa, kuanzia nchani au kwenye kingo za majani. Ugonjwa wa Baka Jani Jekundu unaweza kusababisha majani kupukutika mapema, na hivyo kusababisha mmea kupungukiwa na uwezo wa kunyonya mwanga wa jua, yaani usanisinuru (au usanidimwanga) na hatimae kuathiri mavuno.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hakuna udhibiti wa kibayolojia unaojulikana wa vimelea (viambukizi) hivi. Dawa za kuua kuvu za kikaboni ambazo zimepunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya majani ni oksikloridi ya shaba (2 g/l), haidroksidi ya shaba (2 g/l) na mchanganyiko wa Bordeaux (10 g/l). Utumiaji mmoja wa dawa ya kuua kuvu wakati wa kuanguka kwa petali na kisha mara mbili baina ya muda wa siku 14 ni mzuri katika kupunguza ugonjwa huo.

Udhibiti wa Kemikali

Wakati wote zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kuua kuvu ambazo hupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya majani ni mancozeb, na zile zinazohusiana na dithiocarbamates (2 g/l). Utumiaji mara moja wa dawa ya kuua kuvu wakati wa kuanguka kwa petali na kisha mara mbili baina ya muda wa siku 14 ilionekana kuwa na ufanisi katika kupunguza ugonjwa huo.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na Kuvu (yaani ukungu) aina ya Polystigma ochraceum, ambao huishi na kutengeneza muundo wa ukungu wenye rangi angavu kwenye majani yaliyo hai na pia wanaweza kuishi majira yote ya baridi kwenye mabaki ya miti ardhini. Kwenye majani haya yaliyodondoka, kuvu huunda miundo ya uzazi ambayo itatoa vijimbegu(chavua) katika majira ya kuchipua yanayofuata, wakati hali ni nzuri. Kutolewa kwa vijimbegu huanza na wakati wa kutoa maua na kilele kinapatana na kuanguka kwa petali. Kuvu hii huathiri viwango vya mmea kujitengenezea chakula kwa kutumia mwanga wa jua na tija ya miti.


Hatua za Kuzuia

  • Kama inapatikana(mingi ipo sokoni), tumia aina ya mimea inayostahimili au isiyoshambuliwa sana.
  • Fuatilia bustani mara kwa mara kugundua dalili za ugonjwa huo.
  • Kata matawi yenye maambukizi na yaliyokufa ili kupunguza maambukizi.
  • Ondoa sehemu yenye maambukizi ya mti wa mlozi pamoja na majani yanayooza na sehemu za maua zilizobaki.
  • Tishu zilizoondolewa zinapaswa kuharibiwa kwa kuchomwa moto au kuzika kwenye shimo lenye kina kirefu.

Pakua Plantix