Togninia minima
Kuvu
Ugonjwa huu unaweza kutokea wakati wowote katika msimu wa ukuaji wa mizabibu. Dalili kuu ni michirizi inayotokea kati ya mishipa ya majani, michirizi ambayo hutambulika kwa ubadilikaji wake wa rangi na kukauka kwa tishu zinazozunguka vena kuu (mshipa mkuu). Kwa kawaida, michirizi hii huonekana kuwa na rangi nyeusi yenye wekundu kwa aina ya zabibu nyekundu na rangi ya manjano kwa aina ya zabibu nyeupe. Majani yanaweza kukauka kabisa na kudondoka kabla ya wakati. Kwenye matunda ya zabibu kunaweza kutokea madoa madogo, meusi, yenye umbo la mviringo, madoa ambayo mara nyingi hupakana na mduara wenye rangi ya zambarau ya kahawia. Madoa haya yanaweza kutokea wakati wowote kati ya kipindi cha kutoka kwa matunda na kuiva. Kwenye mizabibu iliyoathirika kwa kiasi kikubwa, matunda mara nyingi hupasuka na kukauka. Maduara yanayotokana na madoa meusi huonekana baada ya kukata sehemu mbalimbali za mzabibu. Aina kali ya Ugonjwa wa Shina la Mzabibu inayojulikana kama apoplexy husababisha na kukauka ghafla kwa mzabibu mzima.
Lowanisha vipandikizi vyenye majeraha sugu kwa dakika 30 kwenye maji moto yenye joto la takriban 50°C. Matibabu haya si yenye ufanisi mara zote na hivyo yanapaswa kutumiwa na mbinu zingine. Baadhi ya kuvu aina ya Trichoderma zimekuwa zikitumika kuzuia maambukizi kwenye majeraha yanayotokana na kupogoa matawi, majeraha yaliyo karibu na kitako cha mmea, na kwenye muunganiko wa sehemu zilizobebeshwa. Matibabu haya yanapaswa kufanyika ndani ya saa 24 baada ya kupunguza matawi (kupogoa) na kisha wiki mbili baada ya hapo.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Mikakati ya kikemikali ya kudhibiti ugonjwa huu ni migumu kwa sababu walinzi asili wa majeraha hawaingii ndani zaidi ya majeraha sugu ya mizabibu ili kuathiri kuvu. Mbinu za kuzuia ndiyo njia bora zaidi ya usimamizi wa magonjwa yote ya shina. Kwa mfano, mapema kabla ya kubebesha vipando, mizabibu inaweza kuingizwa kwenye nta maalum zenye wasimamiaji wa ukuaji wa mimea au mchanganyiko wa dawa za kuua kuvu. Hii huchochea maendeleo ya kuunganika kwa vipandikizi wakati inazuia uambukizaji wa kuvu.
Dalili hizi husababishwa hasa na kuvu/fangasi aina ya Togninia minima, lakini kuvu wengine (kama vile Phaeomoniella chlamydospora) pia wanaweza kuhusika. Maambukizi kwa hakika hutokea katika mizabibu michanga, lakini dalili zinaweza kuonekana wazi kwa mara ya kwanza kwenye mashamba baada ya miaka 5-7. Kuvu (ukungu) huishi msimu wote wa baridi wakiwa ndani ya sehemu ngumu za mzabibu. Kuanzia msimu wa vuli hadi majira ya mvua za msimu wa kuchipua, vijimbegu (viiniyoga) vya kuvu huzalishwa na kutolewa, na kutokea vinaweza kuleta maambukizi kwenye majeraha yanayotokana na upogoaji wa mizabibu. Majeraha kwenye mizabibu yanaweza kuendelea kuwa hatarishi kwa maambukizi kwa wiki kadhaa baada ya kupogoa matawi. Baada ya jeraha lililotokana na upogoaji kupata maambukizi, vimelea huanzisha maambukizi ya kudumu kwenye mti, maambukizi ambayo hayawezi kutokomezwa kwa kutumia dawa za kuua kuvu.