Papai

Muozo wa Kitako cha Shina na Mizizi

Phytophthora spp.

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Mmea kudumaa na majani madogo.
  • Kubadilika kwa rangi ya Kitako cha Shina kuwa kahawia kunaweza kuonekana kwenye tishu za mishipa ya shina au kwenye sehemu nzima ya juu ya mmea (mwavuli).
  • Kuambukizwa kwa mizizi husababisha uoza wa kahawia hadi mweusi kwenye mizizi.

Inaweza pia kupatikana kwenye

8 Mazao
Mung'unye
Zabibu
Mihogo
Tikiti
Zaidi

Papai

Dalili

Dalili hufanana na magonjwa mengi ya mizizi. Majani madogo na yaliyo badilika rangi kidogo, uwekaji matunda duni na kuoza kwa tishu za ndani ni ishara kuu za muozo wa kitako cha shina na mizizi. Mimea au miti iliyoambukizwa inaweza kudumaa na majani machache yanaweza kuanguka mapema. Gome linaweza kuonyesha dalili za kuoza na katika baadhi ya matukio, matone ya gundi huonekana. Sehemu za mkato za kitako cha shina zinaonyesha makovu ya rangi nyekundu-kahawia yenye seli mufu kutoka kwenye shina hadi mizizi. Kikwachu/donda gome hatimaye huzunguka shina, na kuzuia usafirishaji wa maji na virutubisho hadi sehemu za juu za mmea, na hatimaye kuua matawi, kuanzia kwenye ncha. Mimea au miti hufa polepole na inaweza kung'olewa kwa urahisi kutoka ardhini.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Matibabu ya kibayolojia ya kupambana na kuvu yanaweza kufanywa, kwa mfano kwa kuchora vidonda na kupogoa kwa mchanganyiko wa Bordeaux. Matibabu ya kuzuia kwa mchanganyiko huo pia hupunguza mashambulizi. Endapo miti itakuwa imeathiriwa sana, ugonjwa hauwezi kuponywa na ni hatua za kuzuia pekee zinaweza kusaidia kupunguza ukali wake.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi inayochanganya hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Njia bora ya kutibu miti/mimea ni kwa kutumia dawa za kuua kuvu kwa umwagiliaji. Kwa dalili za awali, mwagilia vizuri kitako cha miti na dawa ya kuvu yenye phosetyl aluminium, metalaxyl au methyl thiophanate-methyl. Ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu, zana za kilimo zinapaswa kutakaswa na jiki baada ya matumizi.

Ni nini kilisababisha?

Dalili husababishwa na aina kadhaa za fangasi wa jamii ya Phytophthora. Mara baada ya kuingizwa kwenye shamba, wanaweza kuishi katika udongo kwa miaka mingi na kuwatokomeza haiwezekani. Kuvu hawa hutegemea viwango vya juu vya unyevu wa udongo na hali ya hewa ya unyevu, ya joto kwa maendeleo yao. Mimea au miti iliyo na ugonjwa mara nyingi hupatikana mmoja mmoja au katika vikundi vidogo shambani, huambatana na maeneo yenye upitishaji duni wa maji, mafuriko ya mara kwa mara au umwagiliaji kupita kiasi. Katika mashamba au bustani yenye vifaa vya umwagiliaji kwa njia ya matone, dalili zinaweza kuonekana mara kwa mara kwenye mashina ambayo yaliyoko moja kwa moja chini ya vali, ambapo maji yanakuwa yakitoka moja kwa moja. Njia nyingine ya uenezaji wa ugonjwa huo ni kupitia usafirishaji wa mali ghafi zilizo ambukizwa, kwa mfano wakati wa kupandikiza.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina zenye ukinzani kwa Phytophthora kama zinapatikana.
  • Usisafirishe miche/mimea iliyoambukizwa kati ya mashamba, maeneo tofauti.
  • Usipande katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko.
  • Sahihisha shida yoyote ya mifereji ya maji ambayo inaweza kupelekea mkusanyiko wa maji karibu na shina.
  • Epuka mafuriko ya mara kwa mara na ya muda mrefu ya udongo.
  • Dumisha matandazo ya asili juu ya eneo la mizizi.
  • Hakikisha bustani au shamba halina mabaki ya mimea.
  • Panga uwekaji mbolea wenye uwiano.
  • Ondoa sehemu za mimea iliyoambukizwa au miti iliyokufa na uchome moto.
  • Usitumie mazao mseto ambayo yanaweza kueneza ugonjwa huo.
  • Hakikisha umesafisha vizuri vifaa vya shambani kabla ya kuhama kutoka sehemu zilizoshambuliwa na kwenda kwenye maeneo safi.
  • Hakikisha umerekebisha umwagiliaji kwa njia ya matone ili maji yasiende moja kwa moja kwenye shina.
  • Wakati wa kupandikiza, hakikisha unaweka viungio vizuri juu ya udongo.

Pakua Plantix