Elsinoe ampelina
Kuvu
Kuvu huathiri sehemu zote za kijani za mzabibu, majani, vishina, mashina na kikonyo. Hata hivyo, ni tishu changa na zinazokua kwa haraka ndizo huathirika zaidi. Kwenye majani, madoa madogo ya kahawia hutokea kwenye lamina (ubapa) ya juu. Kadri madoa yanavyoongezeka ukubwa, hatimae yanakuwa yasiyo na umbo maalum na sehemu ya katikati taratibu inakuwa na rangi ya kijivu na tishu zilizokufa. Hatimaye, tishu zilizokufa huanguka, na kusababisha athari inayofahamika kama shimo la risasi. Aina hiyo hiyo ya madoa na vidonda huonekana kwenye mashina na vishina na madoa hayo yanaweza kuzunguka shina/vishina, na kusababisha kutokea kwa vikwachu(vidonda) na kuanza kufa. Madoa madogo, yenye umbo la mviringo na ya rangi ya zambarau pia hutokea kwenye matunda. Taratibu madoa hutanuka na kuonekana yamezama huku yakiwa na rangi ya kijivu iliyofifia mithili ya majivu na kingo za kahawia. Kadri madoa yanavyofunika ngozi, zabibu hunyauka na zinaweza kudondoka au kukauka zikiwa kwenye mashada yake. Madoa ya kipekee ambayo katikati yana rangi ya kijivu iliyofifia mithili ya majivu ndiyo yanatoa jina la kawaida la ugonjwa huu, yaani kuoza kwa jicho la ndege.
Utumiaji wa kimiminika cha salfa ya chokaa au upuliziaji wa dawa za shaba mwanzoni mwa majira ya kuchipua kabla ya vitumba kupasuka, yamekuwa yakitumika ili kuzuia kuenea vimelea kwa kiwango cha juu. Hakikisha dawa za kuua kuvu zinaruhusiwa ndani ya mpango wa uthibitisho wa organia.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Chule inaweza kudhibitiwa ikiwa njia za asili za kilimo zinafuatwa pamoja na matumizi kwa wakati muafaka ya dawa za kuua kuvu ambazo zitakazopuliziwa kwa ajili ya kuzuia. Upuliziaji wa kimiminika cha salfa ya chokaa au mchanganyiko wa Bordeaux mara vitumba vinapopasuka itasaidia kupunguza matatizo ya chule. Dawa za kuua wadudu zilizosajiliwa kwa ajili ya kuzuia uendeleaji wa ukuaji na matunda ni captan, chlorothalonil, na mancozeb. Kupulizia kila baada ya wiki 2 kuanzia wakati wa vitumba vinapopasuka hadi matunda yanapoanza kubadilika rangi.
Dalili zinasababishwa na kuvu/fangasi anayefahamika kama Elsinoe ampelina. Huwa wanaishi msimu wote wa baridi wakiwa katika muundo wa kuvu kwenye vishina na magamba ya mizabibu iliyoathirika. Wakati wa majira ya kuchipua, kuvu huanza kuzalisha vijimbegu (viiniyoga) ambavyo hutolewa na kusambazwa na rasharasha za mvua. Upepo na mvua hubeba vijimbegu vya kuvu hadi kwenye majani au vishina vichanga vinavyokua. Vipindi virefu vya tishu kuwa zenye majimaji (saa 12 au zaidi) na joto la kati ya nyuzijoto 2-32°C husaidia uzalishaji na kuota kwa vijimbegu vya kuvu. Joto na unyevunyevu vinapokuwa vya juu, ndivyo mashambulizi ya kuvu yatakavyotokea kwa haraka na dalili kuonekana mapema. Hali ya baridi hufanya ukuaji wa kuvu kuwa wa polepole. Kupukutika kwa majani na uharibifu wa moja kwa moja wa matunda kunaathiri kwa kiasi kikubwa mavuno na ubora wa matunda.