Athelia rolfsii
Kuvu
Kuvu hushambulia shina, ingawa sehemu zingine za mmea zinaweza kuathiriwa wakati hali ya hewa ni rafiki. Hukua kwa kasi juu ya tishu za mmea na udongo unaoizunguka na kutengeneza utando mweupe, vibonge vya sufi ya kuvu venye umbo la mviringo, mbegu za rangi nyekundu nzito hadi kahawia. Tishu za shina hubadilika kuwa na rangi ya kahawia hafifu na laini, lakini sio maji maji. Katika baadhi ya matukio, shina inaweza kuwa imefungwa kabisa na majani polepole huanza kunyauka na kubadilika rangi kuwa ya njano. Hatimaye, mmea unaweza kukaa au kufa, na safu nzima au sehemu kubwa za mimea iliyokufa zinaweza kuonekana ndani ya shamba. Miche huathirika zaidi na hufa haraka mara tu inapoambukizwa. Mara chache, matunda pia hufunikwa na utando wa kuvu na huoza haraka.
Kuvu wapinzani (mara nyingi pamoja na matibabu mengine) wanaweza kutoa udhibiti fulani dhidi ya vimelea hivi. Kumbuka kwamba matokeo hutegemea sana aina ya mazao na hali ya mazingira. Baadhi ya viumbe vinavyotumika sana ni Trichoderma harzianum, Trichoderma viride, Bacillus subtilis, Streptomyces philanthisome, Gliocladium virens na baadhi ya spishi za Penicillium.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Matumizi ya vifukizo vya udongo vyenye wigo mpana kabla ya kupanda hutoa udhibiti mzuri wa kuvu. Bidhaa zinazotokana na metam sodiamu zinaweza kutumika kutibu vitalu vya mbegu au mashamba kwa mazao ya thamani.
Dalili husababishwa na fangasi Athelia rolfsii, anayejulikana pia kama Sclerotium rolfsii, na hivyo kuleta jina la kawaida la ugonjwa huo. Kuvu huyu huishi kwa msimu mzima katika udongo au kuambatana na uchafu wa mimea. Husababisha magonjwa kwenye aina mbalimbali za mazao ya kilimo na bustani (dengu, viazi vitamu, maboga, mahindi, ngano na karanga, kwa kutaja machache). Katika hali rafiki, ana ukuaji wa haraka sana na anaweza kutawala tishu za mimea kwenye au karibu na mstari wa udongo ndani ya siku chache. Udongo wa pH ya chini (3.0 hadi 5.0), umwagiliaji wa mara kwa mara au mvua, upandaji wa karibu karibu/msongamano na joto la juu (25 hadi 35 °C) husaidia mzunguko wa maisha wa kuvu na mchakato wa kuambukiza. Kwa utofauti, udongo wenye chokaa na pH ya juu kwa kawaida hausababishi matatizo. Usambaaji hutegemea mzunguko wa udongo na maji yaliyoambukizwa, zana na vifaa vyenye vimelea, pamoja na mazao ya mimea na wanyama yaliyoambukizwa (mbegu na samadi).